Window gani nzuri kwa ajili ya fundi simu upande wa software?

Window gani nzuri kwa ajili ya fundi simu upande wa software?

sina uhakika labda kama unajua jina la box tucheki
Box ni UFI BOX
37193486-FB80-4133-8B7E-63A0870C9087.jpeg
 
Wakuu naomba kujuzwa kati ya window 7 na 10 ipi ni nzuri kwa ufundi simu upande wa software ninazo box na sio crack
Kwa upande wa software hasa za kuflash hakuna windows ambayo itakidhi haja zote hasa kama unatumia hdd.

Nimewahi tumia windows 7, 8, na 10 zote 64bit kwenye hdd kila windows ilikuwa na shida zake, karibia kila miezi miwili hadi mitatu nilikuwa naweka windows mpya.

Kwa windows 8 na 10 simu za zamani hasa nokia muda mwingine wakati wa kuflash windows ilikuwa inaleta blue screen error, ila kwa windows 7 ilikuwa vizuri.

Baada ya ujio wa windows 11 naona changamoto nyingi zimepungua.

Baada ya kununua ssd kwa sasa nimejaribu windows 10 na 11 zote sijaona shida yoyote. Kuna baadhi ya hdd naona haziko vizuri kwa kuwekewa windows ninayo moja nikiweka windows box la ufi software yake haifunguki ila application zingine zinafunguka vizuri.

Kuna software ya kutest ram, hdd na nk kwenye kompyuta na inakupa matokeo ya kila utendaji wa kifaa kilichoungwa kwenye kompyuta yako na inatoa pendekezo kama unataka kubadilisha vifaa vilivyomo na kuonyesha vilivyobora na vitakavyokupa matokeo mazuri.

Software inaitwa userbenchmark itumie kwanza kuangalia kama hardwares za kompyuta zako ziko sawa.
 
Back
Top Bottom