Wewe kinachokushangaza ni nini? Watu kuwa wengi kwenye kozi hiyo, au vyuo vingi kutoa kozi hiyo. Umesema watu wa biashara ni nafuu wanaonyesha kukomboa Taifa, nakubaliana na wewe, ila wajua kama biashara ya sasa haiendi bila Technologia ya Mawasiliano? Umesema wanachojua wengi ni kuformat tu... Ok acha kila mmoja aelewe kutokana na uwezo wa kichwa chake, Umesahau kama umeweza kuposti comment yako humu kwa kwa ajili ya IT, Matumizi ya kutuma pesa popote ulipo kwa kutumia simu huoni kama ni msaada kwa jamii? Waweza chukua pesa muda wowote kwa kutumia Automated Teller Machine (ATM) aka Cashpoint, unafikiri ni Commerce ndo inayofanya kazi hiyo? Huoni ni jinsi gani IT inavyosaidia kuelimisha kisiasa, kiuchumi, na hata kiutamaduni...? Umepost hii status bila kufikiria au? Nahofia kuwa waweza kuwa um1 kati ya watu ambao wanaofikiri baada ya kutenda...! Fungua macho yako mkuu, Au kuna IT aliyekuformatia PC yako na kukupotezea DATA...? Basi ukiona hivo jua huo ndo uwezo wake yeye. Sidhani kama kuna kozi yeyote ile duniani ambayo ukisoma uelewa wa watu wote unalingana na sidhani pia kama vyuo vyote vinalingana kwa uwezo wa kufundisha... Wewe ulipokuwa unasoma, au kama bado wasoma, Je wote mwaelewa sawa, au mlikuwa mkielewa sawa?
Ushauri wangu, Fikiri kabla ya kutenda, au kunena.
Asante