Ms Judith
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 2,563
- 929
1.
Nimepata wa thamani, ni hakika si majungu,
Mwingine sitatamani, nimefunga moyo wangu,
Sikupotea ramani, nimezikubali pingu,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
2.
Kila nionapo wingu, sikosi kuona mbingu,
Huwezi ingia mbingu, bila liingia wingu,
Wingu liko na mbingu, mbingu zina mawingu,

3.
Hayawi hayawi yawa, thelathini siku zawa
Sio nyingi kama chawa, zi nyepesi kama buwa,
Kwa sala na zote duwa, maombi yamejibiwa,

4.
Tangu tulipozianza, ndoto za baba na mama,
Ni mengi tumejifunza, tukabakiza kuhama,
Na sasa twende kufyonza, tamu iliyofichama

5.
Mwaka ule si karibu, subira ndio mtaji,
Tele hayo majaribu, yasiyopozwa na maji,
Imara kama bawabu, makini kama hujaji,

6.
Nyakati nayo majira, na zama zimetimia,
Mapenzi haya imara, silaha kuu ya ndoa,
hazijalishi ngawira, mapendo tumekamia,

7.
mpira ulipoupiga, niliepa nisidake,
kwa mengi ulinikoga, japo hunayo makeke,
na sasa nimejibwaga, hirimu wangu nishike,

8.
za mwizi hazikawii, zetu walizikamia,
pamoja nayo bidii, ya maombi kuazimia,
agizo sasa kutii, la ndoa na familia,

9.
asante mpenzi wangu, kimasomaso menitoa,
mapendo kama uchungu, kwa machozi nimeloa,
lishike vizuri rungu, kwako nimeshajitoa,

10.
tuijenge hiyo nyumba, yenye kujaa vicheko,
watoto nao kuumba, mbinguni tupate heko,
wala tusije kuyumba, kwani tunao upako,

11.
udumu cha nyumba kichwa, mimi ni wako ubavu,
bidii ipite mchwa, ushinde wote uchovu,
nyuma tusije kuachwa, kwa Yesu uko wokovu

12.
Asante wote wapendwa, kwa maombi nazo dua,
Ni kweli hamkushindwa, shetani kumkemea,
Upendo uliopandwa, hitaji kuu la ndoa,

wapendwa,
pamoja na kuzidiwa na majukumu mengi kikazi, Mungu aliyajibu maombi tena vizuri sana. mchumba wangu anaitwa Naiman na ni mzaliwa wa Iringa. kama mjuanvyo masuala haya yana logistics nyingi na hivyo kukamilisha yote yaliyo ya muhimu inahitaji muda. hadi sasa mengine hayajakamilika. hapo katikati nilibahatika kupata scholarship ya kuripoti chuoni september mwaka huu na hivyo mtaona kuna kibarua cha kupangilia mambo hapo, kupata ruhusa na likizo ya masomo kazini na kuandaa harusi na wakati huohuo kutakiwa kuwa chuoni. so baada ya panga pangua, natarajia kwenda chuoni kwanza na kisha kurudi nyumbani november kwa ajili ya kufunga ndoa.
Mungu awabariki sana,
Glory to God!