Wingu na Mbingu

Dada Judy we hongera, nimefurahi kujua
wacha nandae kamera, kumbukumbu jiwekea
tigo mpe bila kura, kama livyokwishatuambia
mapenzi yawe imara, nje asahau tokea!
Lol...

hayo mambo ya sodoma mpendwa, achana nayo na Muogope Mungu,

Glory to God!
 
Hongera sana MJ.Nakutakia kila la heri katika maandalizi ya harusi
 
1. Kumpata mwenza bahati, siku hizi ni adimu,
Nakupongeza kwa dhati, machangu sikuhujumu,
Shika sana lake shati, peke yake ndo adhimu,
Hongera na Mungu akujalie uvumilivu na upendo.

2. Maisha kama safari, uchumba kituo kimoja,
Mwanzo hauna shubiri, wambea najikongoja,
Chai yenye sukari, maisha yenye faraja,
Hongera na Mungu akujalie uvumilivu na upendo.

3. Uvumilivu muhimu, mapenzi geuka ndimu,
Kila siku si karamu, waweza ishiwa hamu,
Tabia mfano wa bomu, tahadhari ufahamu
Hongera na Mungu akujalie uvumilivu na upendo.
 

kwenye nyekundu, you have made my day,.................. kwenye blue, its noted and saved for future use,................ ila fumbo la mbingu na wingu linahitaji watu wa bakita waje watudadavulie....................... manake hata gaijin kajaribu ila naona bado bakita wanahitajika zaidi hapo,.............. by the way, hongera sana mwali wetu, ................... ila nov mbali mno jamani si na kiu itaisha??.............. fanyafanya basi angalau uirudishe nyuma hiyo shughuli japo miezi miwili, eeh??.................. tafadhali mpendwa............... au mwenzetu huna haraka "kufyonza tamu iliyofichama"??...............

Mungu akutangulie katika mipango yako.................. imebidi tu nikuombee aisee japo ningetamani hapo kwa Naiman pasomeke "AK"............... teh teh..................
 

mkuu, kumbe na wewe umo??................ hongera sana kuwakilisha!!....................
 

...Hongera sana MJ ila kumbuka "
An Ounce of Action is Worth More than A Ton of Theory or Shayiri la Beti 25"

.......Simple like that...GIVE LOVE....GET LOVE....The more you love, the more you get love

Ile misimamo yako ya kubalehe na kisingo iweke pembeni kidogo....usijemdindia Naiman mpaka pambio la kusifu na kuabudu ndio "Rungu" litangwe .....hahahaaa

BTW: Ni jambo jema sana mtu kupata mke/Mume....hakika ni jambo jema na Hongera tena
 


Ndoa zingine maziwa, huishi wewe kunyonywa,
Miaka inavyozidia, wazidi kudanganywa,
Hata kile kilojaa, huishia kumumunywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Kwa dini au sheria, harusi yenu hufanywa,
Ahadi mtazitoa, mkatae kusengenywa,
Na mafunzo mtapewa, na wazazi mkakanywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Ukweli hujifichua, wakati mnap0ofinywa,
Maslahi kupungua, kila pembe mnaminywa,
Hali zinapotitia, watu rahisi kugawanywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Ndugu na hao jamaa, ya uongo hutawanywa,
Hubakia kuvizia, yatangazwa yasiyofanywa,
Na mitego husambaa, wategwe wasiokanywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Hodari walioamua, milele kutokugawanywa,
Kisha wakajititimua, wasiwe watu wa kunywa,
Fedha kudundulizia, waache tena kunyonywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Kuwekeza wakitua, vinginevyo wakatonywa,
Mke anapoamua, hataki tena kunyonywa,
Mbele akavichukua, huku mume anasonywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Mme chumvi hudaiwa, na chake kikamenywa,
Bahili mke akawa, sio wa kumumunywa,
Mme nguvu hulegea, asitake kutekenywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Ndoa jambo maridhia, ila pasiwe kunyonywa,
Nikahi kitu murua, mtu asiposengenywa,
Nyumba hujititimua, na watu msipogawanywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa
 

nimekupata vizuri sana mpendwa

Mungu akubariki sana
 

Mie nimefurahi sana Judith maana umeweza kuuthibitishia umma wa JF kwamba ile thread yako ya mwanzo haikuwa usanii. Sasa tunasubiri kwa hamu kuu mtutangazie harusi, harusi ambayo nadhani itakuwa ya kwanza kuhudhuriwa na wanaJF wengi. Kila la heri katika safari yenu.
 

nashukuru sana mpendwa, bila shaka sitawasahau wote jamvini. aliyedhani ni usanii tusichoke kumuombe. Mungu akiwa upande wetu hakuna atakayekuwa juu yetu. mkononi mwake tunapata kushinda na zaidi ya kushinda.

Glory to God!
 
Hongera sana miss Judy
Mungu azidi kukuongezea
Nguvu na baraka zaidi katika
Mipango yako...

My dear nimeanza kulifikiria
hilo gauni la harusi hahaha lol
Kila lakheri na masomo yako pia.
 
9.
asante mpenzi wangu, kimasomaso menitoa,
mapendo kama uchungu, kwa machozi nimeloa,
lishike vizuri rungu, kwako nimeshajitoa,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!

yaani alishike vizuri rungu
kwa sababu ana kazi kubwa ya kukubikiri au.......................................
 
nashukuru sana mpendwa, bila shaka sitawasahau wote jamvini. aliyedhani ni usanii tusichoke kumuombe. Mungu akiwa upande wetu hakuna atakayekuwa juu yetu. mkononi mwake tunapata kushinda na zaidi ya kushinda.

Glory to God!

tatizo langu ni kuwa ulikuwa wapi hadi ukashtuliwa na Pakajimmy?..........................
 
Hongera sana miss Judy
Mungu azidi kukuongezea
Nguvu na baraka zaidi katika
Mipango yako...

My dear nimeanza kulifikiria
hilo gauni la harusi hahaha lol
Kila lakheri na masomo yako pia.

asante sana mpendwa
nawe nakutakia kila la heri kwa kila mkono wako unalotia bidii kulifanya
Mungu akubariki sana
 
tatizo langu ni kuwa ulikuwa wapi hadi ukashtuliwa na Pakajimmy?..........................

Nilikuwa nafikiria the same...................

wapendwa, majibu ya maswali haya yako kwenye post no. 88 ukurasa wa tano na ni kama ifuatavyo:


post hii inapatikana https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/148512-mchumba-wa-miss-judith-5.html
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…