Wingu na Mbingu

pole na maandalizi dada. sasa ma-best gal nguo tunashonesha lini,manake mie fundi wangu wa manzese yuko busy ibidi booking mapema. ama shem anatuagizia ulaya? navaa size zero,lol
asante sana mpendwa nawe nakutakia kila la heri kwa kila mkono wako unalotia bidii kulifanyaMungu akubariki sana
 
pole na maandalizi dada. sasa ma-best gal nguo tunashonesha lini,manake mie fundi wangu wa manzese yuko busy ibidi booking mapema. ama shem anatuagizia ulaya? navaa size zero,lol
Tusubirie tu naona atatuletea ready made
 
hahaha, kwa kweli kwa sasa sijaanza kupangilia masuala ya nguo, hata rangi ya harusi sijaichagua, lol! nimetingwa na mambo mengine chungu mzima, tuombe Mungu taratibu tutafika tu wapendwa

stay blessed!
 
hehehe, hebu fanya mipango bana manake tushajiwahia u-bestigeli hapa manake na sie tuna hamu ya kupigwa picha atii! usijali mamii, yeye aliyeianzisha kazi hii ndani yako ataimaliza yeye mwenyewe na utashangaa mambo yatakavyoenda sawa bila nguvu nyingi.

hahaha, kwa kweli kwa sasa sijaanza kupangilia masuala ya nguo, hata rangi ya harusi sijaichagua, lol! nimetingwa na mambo mengine chungu mzima, tuombe Mungu taratibu tutafika tu wapendwa

stay blessed!
 
loh, maneno mazito haya ya faraja dadangu. kwa hakika sina wasiwasi kabisa na naamini tutavuka salam. Mungu akubariki sana
 
Karibu ma naimani,karibu kwa ukubwani,
Ndoa naibarikini,bado sio kanisani,
jitie we kitanzini,mumewe umtunzeni,
Nendeni mkazaane,Mlijazeni dunia,

maombi uliyaomba,magoti ukayapiga,
ulitaja kwa muumba,ili akupe we mwanga,
wetu yeye maharuba,kakupa ka ulopanga,
Nendeni mkazaane,Mlijazeni dunia,

Ya kwanza ni kuzaliwa,ya pili ndio harusi,
Ya tatu utajaliwa,kifo nacho sio hasi,
Mpende wako mpedwa,kwa sana sio kiasi,
Nendeni mkazaane,Mlijazeni dunia,

Hongera ninazirusha,Judi wetu wa hekima,
Kwa hapa ulilirusha,wote tukatoa neema,
Mungu ataliwezesha,kwani yeye ni wa nema,
Nendeni mkazaane,Mlijazeni dunia......

Hongera Miss Judith.....Umediriki kuwa wa kwanza kama Paka Jimmy aliposema...wengi wakipata hupotea bila kurudisha what they achieved...
 
Hongera wetu mrembo, faraja nakutakia
Kaivae hiyo nembo , ya Mrs kwenye ndoa
Uviepuke vikumbo, na mazonge ya dunia
Pokea wangu wimbo, kheri ninakuombea

Akikuita laazizi , honey nawe itikia
Myakoleze mapenzi, msije yachakachua
Akiomba tangawizi, usije mcheleweshea
Usimtie simanzi, akachukia dunia

Tabasamu mpatie, kila akikuangalia
Atakacho mridhie, cha halali na sawia
Aibu msitirie , usiwe kiguu na njia
Vitamu umpikie, mapenzi yatazidia

Mpendane akupende, mema ninawaombea
Ndoa nje msiende , sumu ikaja ingia
Mlishane peremende, usiku ukiingia
Penzi lenu mlilinde, huu ni wangu wosia

Ndoa sio lelemama, yataka ujiandae
Sahau yalo sinema, uhalisia uvae
Jiandae na zahama, subira ndio siriye
Sikuombei kukwama, nakutaka ukomae.

Kalamu ninaiacha , wino umemalizika
Kapake rangi za kucha, umngoje muhibaka
Usije badili bucha , nyama nyengine kutaka
Nitakuja piga picha, hiyo kazi naitaka.

Hongera Miss Judith na nakutakia maisha mema ya ndoa wewe na mwenzi wako na penzi lenu lidumu daima. aaaaaaaaaaaaaaaaaaamen!
 
mpwa kuna wakongo nasikia wanapaka hadi kucha...sasa Miss JF wetu sijui mmewe atampaka kucha au Wakongo watamsaidia kwa hili?
 
mpwa kuna wakongo nasikia wanapaka hadi kucha...sasa Miss JF wetu sijui mmewe atampaka kucha au Wakongo watamsaidia kwa hili?
Mpwa mie waifu wangu simpeleki kwa mkongo hata siku moja! akisisitiza sana namng'olea mbali hayo makucha yake.
 
mie wangu kucha akilala nazikatakata kwa sana tu...
Mkongo anamkata mdada kucha unakuta mguu wa mdada kauweka kwenye zipu ya suruali bana! Khaaa kama miguu inapata ujauzito hawa wadada zetu wangekuwa na maguu pacha kibao kwa wakongo.
kudadeki! hakatwi waifu kucha kwenye himaya yangu.
 
Basi hujajua yote,wanakatwa kucha,kusuguliwa miguu.kukandwa mpaka mapajani yaani vurugu tupu na akitoka hapo anaenda kusuka kwa mmasai asiyevaa chupi na kichwa kuwekwa mapajani akiangalia mkia we acha tu urembo kazi mjini lol! Na hapo bado mpaka kucha rangi wa mtaani hahaha!
 
Basi hujajua yote,wanakatwa kucha,kusuguliwa miguu.kukandwa mpaka mapajani yaani vurugu tupu na akitoka hapo anaenda kusuka kwa mmasai asiyevaa chupi na kichwa kuwekwa mapajani akiangalia mkia we acha tu urembo kazi mjini lol!
hehehe kamanda hapa unauwa soko la watu sasa. Hivi kuna greti thinka kweli ataruhusu waifu wake aende kwa mmasai au mkongo baada kusoma hii post yako?
 
hehehe kamanda hapa unauwa soko la watu sasa. Hivi kuna greti thinka kweli ataruhusu waifu wake aende kwa mmasai au mkongo baada kusoma hii post yako?
Mi nilimpeleka shemeji yako kwa wamasai pale ilala baada ya kuona mazingira nikatoa laki asukwe na mademu we acha tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…