PreGE2025 POTOSHI Witara akimwaga machozi baada ya kuliwa kichwa na wajumbe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
anaandika Hilder Newton:

Maccm ni vilio kila kona maana majina yamefyekwa

Wanasema Idd Amin Mama tayari anaorodha ya wagombea Ubunge ambao anawataka wale ambao walikuwa wanamkosoa na wale ambao anahisi sio wake majina yamefyekwa.

Haya mliokatwa majina njoeni tuungane kudai #NoReformsNoElection
 
Amekatwa na kikao gani? Maana mchakato unaelekeza wajumbe kupiga kura na kupendekeza majina matatu ya wagombea ambao watapelekwa kwenye kamati za siasa za wilaya na mikoa, kisha mapendekezo ya mkoa yatawasilishwa mkutano mkuu.

Lakini katika hatua hizo zote, yale majina matatu yanayopelekwa ni lazima yajumuishe na mgombea anaetetea kiti chake kama amegombea tena. Sasa ukisema amekatwa na Kamati ya wilaya inakua ngumu kukuelewa.
 
nenda tweeter ..... watu wana watu wao ndani ya vikao wanatoa taarifa.
 
nenda tweeter ..... watu wana watu wao ndani ya vikao wanatoa taarifa.
Swali langu ni kikao gani? Maana kikao kinachoweza kutamka kwamba aliekua anashikilia kiti ameenguliwa kwenye mchakato ni kikao cha mwisho (kamati kuu).

Hivi vya wilaya na mikoa vimepewa mamlaka ya kushauri tu kulingana na kura za wajumbe kuwa inaonekana aliekua mbunge hana mvuto tena, kwahiyo kura za wajumbe ziheshimiwe. Mkutano mkuu utapitia hayo maoni na kisha kukubaliana nao ama kutokubaliana nao.

Lakini msisitizo ni kwamba, hata kama mgombea huyo atapata kura sufuri, ni lazima jina lake lipitishwe kati ya majina matatu yanayopelekwa kujadiliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…