Mwita Waitara ni mwanasiasa kutokea nchini Tanzania. Kwa sasa Waitara ni mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini anayemaliza muda wake kwa tiketi ya CCM, awali amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Ukonga mwaka 2015 kupitia tiketi ya CHADEMA.
Madai
Julai 12, 2025 kumeibuka kipande cha video kikimuonesha mbunge wa Tarime vijijini anayemaliza muda wake, Mwita Waitara aikimwaga machozi mbele ya waandishi wa habari na kuelezwa kuwa tukio hilo linakuja mara baada ya yeye kukatwa jina na wajumbe.
Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache tangu mchakato wa kutafuta wagombea wa ubunge, udiwani na baraza la wawakilishi kwa chama cha mapinduzi kuzinduliwa rasmi.
Uhalisia wa Taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa kipande hicho si cha hivi karibuni.
Kipande cha video kinachomuonesha Mwita Waitara mbunge wa Tarime Vijijini akilia si ya mwaka 2025 na haihusiani na mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2025.
Kipande hicho cha video ni kutoka katika sehemu ya hotuba aliyoitoa WaitaraMachi 28, 2023 alipokuwa akizungumzia adha ya migogoro ya mipaka Jimboni mwake.
Aache kulia lia hizo hela alizokusanya kwa kipindi chote cha kulamba asali akajiajiri.......afadhali yeye hata ana mtaji wa kuanzia maisha mtaani.....vijana wanatoka vyuoni watupu wanapambana mtaani.....
Hawa watu wabinafsi sana, hawajawahi ongelea vilio vya wa Tanzania kila siku, jitu Kiko nje huru, Lina pension, linalia? Hivi hawa wanajua 1% of our hustles ? Wanaume ni wachache wana