PreGE2025 POTOSHI Witara akimwaga machozi baada ya kuliwa kichwa na wajumbe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
KINACHONICHEKESHA NI KUWA WANAOSEMA NO REFORMS NO ELECTION NDIO WANAOONGOZA KUJADILI NANI KAPITA KWENYE KURA ZA MAONI NA NANI HAJAPITA.

Ndugu zangu huwa mnasema hakuna uchaguzi mwaka huu sasa hizo kura za maoni mnazotuhabarisha zinahusiana na nini.

Maana naona mnafuraha kabsa mkiona wale msiowapenda wamekosa.

JITAHIDINI MJUE MNAPAMBANIA NINI ITAWASAIDIA SANA.
 
Watu wa mara hutaliagi kifala hivyo mbele za watu hata kama umepitia ugumu gani......Mwita umetuabisha bna
 
Mkurya ana machozi ya karibu sana,
Machozi yaliyokaribu kwa hawa majamaa ni yale ya hasira kali inayodai na inayotaka kulipiza kisasi fasta au kutembeza kichapo kitakatifu. Sio machozi ya kutaka uonewe huruma. Ndo mana wadau wamemshtukia huyu mwamba.
 
Machozi yaliyokaribu kwa hawa majamaa ni yale ya hasira kali inayodai na inayotaka kulipiza kisasi fasta au kutembeza kichapo kitakatifu. Sio machozi ya kutaka uonewe huruma. Ndo mana wadau wamemshtukia huyu mwamba.
CCM nao wajitafakari sasa, unamteua mtu kama huyu kuwa naibu Waziri kweli? Au ilikuwa Janja kuwavuta viongozi wengine wa CDM wahamie CCM
 
Moderators Active naomba ufafanuzi: Ni potoshi kweli? Waitara kweli hajakatwa?
 
nipe mrejesho, matokeo bado? maana nyinyi uchawa umewapofusha kuona ukweli.....
Uchawa upi unaouzungumzia hapo Ndugu, mimi nimeelezea mchakato wa upitishaji majina wa CCM na kuhoji kama jina limekatwa ni kwa kikao gani?

Kwahiyo humu ndani mtu asipokubaliana na wewe basi anaitwa chawa? Ulichopaswa kueleza ni kwamba amekatwa na kikao fulani na kwa misingi hii.

Kuhusu matokeo sina taarifa yoyote, lakini ninachoelewa ni kwamba utaratibu uliowekwa na CCM ndio ulitakiwa kufuatwa, kama ameondolewa basi itakua kuna mahali taratibu za chama zimekiukwa, ama kuna mabadiliko ya kanuni yalifanyika hivi karibuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…