Mkuu nngu007, tufuatane kwenye RED! Ukishasikia wanasema kwenye nchi fulani hakuna demokrasia basi ujue kuwa interest zao zimebinywa na wanatafuta njia ya kuiangusha serikali husika, Hata Libya, Iraq na kwingineko walianza kwa style hii!
Kiongozi Imara mwenye kukataa sera zao ama alieamua kufuta mikataba mibovu kama Hugo Chavez na Rais wa Equatorial Guinea, Ghadaffi, Mugabe et al huwa wanawaita madokteta na kuwa hawafai kutawala badala yake viongozi dhaifu wenye kuruhusu rasilimali zao kukwapuliwa huwa wanasifiwa kuwa ni viongozi bora wapenda demokrasia...
Typical style ya CIA, huwa inawalisha chambo kisha wanawanasa kwa vijizawadi vya kufunguliwa a/c zenye dolla nyingi ughaibuni! Hapa kwetu tayari kunawatu wamewekewa mabilioni Uswis, siku wakianza kutumia hizo dola na deal lisifanikiwe lazima watazitema tena kwa mbwembwe kwa kufreez a/c husika!
Tayari mwenye umeshaainisha kuwa makampuni ya kimarekani ndo yaliyomuwekea fedha huyo dogo! Haya yasingetokea kama baba yake asingefuta mikataba ya uchimbaji mafuta na kuwapatia wachina...
Kumbuka kuwa CIA siku zote huwa wanaanza kwa kuwatenganisha na kuwagawa Jamii kwa kuchochea uasi thru NGOs, wamefanya hivi na kufanikiwa sehemu nyingi duniani zikiwemo za kiarabu, hii inakuwa ni hatua ya kwanza, Hatua ya pili huwa wanawatuma Jacko! ambao huwaandalia viongozi vifo vyenye kufanana na ajali! Hatua hii ikishindikana huwa wanakuja na slogan ya no fly zone...mwisho wa siku wanakutumia marine ...
Mkuu, hatakama wewe ni pro west basi jaribu kufunua macho maana haya mambo hayafanyiki wa kificho tena...