With $11bn Bagamoyo port, Tanzania prepares to take on EA hub Mombasa


Asante, Tuwe wazalendo, pale serikali inapofanya vyema tuwape hongera zao, kwa hili hongera Kikwete..
 

Point mkuu ila wakati mwingine ukiangalia mambo yanavyokwenda nchi yetu hii unaweza kulia maana hizo bandari zilizopo tu zimetelekezwa inajengwa nyingine ya kiwango maana siamini kama mizigo yote inatakiwa ipite Dar kwani kuna mingine ingeweza kupita hata Mtwara na Tanga kulingana na wapi inakwenda pia hata urasimu usingekuwepo bila kusahau FOLENI ya magari Dar maana tunaangalia tu magari yaendayo kasi pia hata idadi ya magari yanayokuja Dar kufuata mzigo nayo yana mchango kwenye foleni pia. Sie ni wazee wa Trial and error
 

Hope Bagamoyo port itakuwa kubwa kuliko ya Lamu, kwani hii itakuwa kubwa kuliko port yoyote katika ghuba ya gulf, ukiangalia yaweza kuwa katika Top Five au Ten ya Dunia ukitoa zile Bandari kubwa nne za China/Hong Kong Singapore. Kimsingi ni project nzuri provided tungelikuwa na uhakika na ToRs zake
 
watz sijui tuna nini maana utafikiri hii habari ndio imejulikana leo! Hili suala limezusha mjadala mkubwa nchini na nje ya nchi na katika conditions za ujenzi wa huu mradi imeonekana wazi kuwa unawasaidia zaidi wawekezaji mpaka Mh. Waziri aliulizwa na kusema aulizwe meneja mkuu wa TPA. Tuwe wakweli hii babdari inajengwa na wachina kwa 100%, wataiendesha kwa miaka 50 nahaitakiwi kuendeleza bandari kwenye umbali wa km200 ambazo hizo zinahusu Tanga na Dar es Salaam.
Anayeona anafurahia na kufaidika na baadhi ya hayo masharti basi awe wa kwanza kusema "
Tanzania prepares to take on EA hub Mombasa" na sio "China prepares to take on EA hub Mombasa"
 
Siku tukipa viongozi na sio watawala wazalendo walio jitoa kwa niaba ya wa tz tena wenye macho ya kuona fursa za kiuchum zinazotuzunguka Basi kuna nchi itaanzisha vita nas kwa sababu ya wivu tu!
 
Mkuu hizo a/c za nje wasiliana na Zitto akupe details zaidi, MNCs tena za nchi za magharibi ndo zimewafungulia a/c hawa tunaowaita mafisadi! Ukiona ghorofa zinapanda ujue kuwa ni kiasi cha mrejesho wa Barrick et al kwa hawa tuliowapa dhamana ya kututawala...
EPA iliasisiwa na kuliwa na Agent wa CIA bw Daud Ballali... vitu vingine unaweza kusema wanasingiziwa lakini sisi tuliokuwepo wakati ule wanamfuta kazi Dr Rashid pale BOT tulishuhudia party ya nguvu ikifanywa na hawa makuwadi...Hawa akina maganga walilambishwa asali wakatamani kuchonga mzinga kabisa... sasa hivi upofu umewatanda ndo maana hakuna cha prof wala asiesoma wote wanaonekana sawa tu, kila mmoja yuko bize kupiga deal ...hushangai mama Tibaijuka kuidhinisha Hati ya yule mmiliki wa mbuga ya saadani tena kwenye korido? nae pia ni miongoni mwa EHM kwa taarifa yako...JK ana kazi ya ziada maana amezingirwa na moles! Lowassa ilikuwa lazima wamtimue maana haaminiki! Aliwahi kuharibu deal la City Water kama mtakumbuka...
 

Kwa taarifa tu ni kuwa mradi wa kujenga bandari ya Lamu ulizinduliwa rasmi mwaka jana mwezi machi na gharama yake ni zaidi ya US$ 23 bilioni. Mradi huo ndiyo mkubwa kwa Afrika na utajumuisha ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta na reli itakayounganisha Kenya na Sudan ya Kusini.

BBC News - Lamu port project launched for South Sudan and Ethiopia
 
Last edited by a moderator:
Move ya kujenga bandari mpya ni sahihi Dar itazidiwa kabisa na mizigo ifikapo 2017, lazima kuwe na bandari ya pili by then
 
Hivi mkuu nngu007 thamani ya bandari inayojengwa Bagamoyo ni $11 million au 1.1 million?
Ni $11 bilion sio Millions, hiyo unayosema hata CRANE za kisasa kwa bandari haitoshi kununulia, kwani jumba ya yule mchungaji ni dola millions ngapi?
 
"China inapotoa mkopo, kuweka sharti kwa mkopaji na kutoa kitu kitakachoinusha na kutoa
mfano wa nchi ya Angola, ambayo ilipewa mkopo kwa sharti la kupatiwa visima vya gesi, hivyo
ni lazima Serikali ya Tanzania imetoa sehemu ya maliasili zake kwa mkopo huo",
zitto kabwe gazetti la Rai
Imeandikwa na Na Charles Mullinda
Alhamisi, Januari 17, 2013 06:16
 
Habari njema kwa wakazi wa Bagamoyo na maeneo jirani haswa ikiwa ili kile chuo cha uvuvi (Mbegani) kitaendelevya na sio kufa kama kilivyo sasa
 
Move ya kujenga bandari mpya ni sahihi Dar itazidiwa kabisa na mizigo ifikapo 2017, lazima kuwe na bandari ya pili by then

kwani lazima ijengwe nyingine wakati tuna bandari ya tanga na mtwara kwanini hizi bandari yasipanuliwe na kufanyiwa marekebisho kadhaa ili hizo pesa zingine zitumike katika kujenga nyumba za polisi ,walimu,madaktari na wanajeshi mukandala ulikua wapi ungemshauri dhaifu
 

Uko sahihi mkuu lakini, ukweli ni kwamba pamoja na ukubwa wa mradi wa Lamu, lakini Bandari ya Lamu itatumia $3.5Billion pekee na zilizobaki zitaelekeza kwenye accompanied project. Kimsingi kwa maelezo ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo TEUs 20million, maana yake inaifanya hiyo bandari kuwa kubwa kuliko zote Afrika (yaani kuizidi Durban na ile ya Morocco) na eneo lote la Ghuba. Kimsingi ujenzi wa bandari hiyo ya Bagamoyo ni pigo kubwa sana kwa kenya kwani kutapelekea aidha kuchelewesha return ya mradi au kusitisha baadhi ya miradi inayohusiana kwa vile wakati wa estimates zao walizingatia kuwa hakutakuwa na Bandari shindani ya aina yake kwa kuwa bandari ya Lamu automatically ingeliiodhoofisha Bandari ya Dar, lakini sasa Bandari ya Bagamoyo itaidhoofisha bandari ya Lamu na Mombasa kwa kuwa Bagamoyo itakuwa Hub kwa zile Panamax ships. Kwa kifupi hii miradi miwili ni mfano wa ile game maarufu ya Prisoner's dilemma iliyochezwa baina ya Boeing na Airbus kama mipango yao ingekuwa inajulikana kabla.
 
Tatizo ni kwamba hatujui au hatuna uhakika wa Terms of references za ujenzi wake, vinginevyo ujenzi wa Bandari kubwa na ya kisasa kama hiyo ni sahihi zaidi kwa nchi kama Tanzania ambayo inazunguukwa na Land locked countries nyingi. Uju hizi habari za bandari wakati mwingine ni kama biashara ya mabenki ilivyo, ikifilisika Bank moja, na nyingine huathirika kutokana na withdrawal, vilevile katika bandari meli na wafanyabiashara wakishajiridhisha kuwa bandari A ni hub, basi bandari B ilie. Ujenzi wa Bandari ya Lamu kimsingi ulikuwa unaua bandari ya Dar (strategically) na kuhamisha wafanyabisha wote wa central Afrika kutumia aidha Lamu au Mombasa kutokana na uwezo wa kupokea meli kubwa na ufanisi wa utoaji mizigo. Hivyo ujenzi wa hiyo Bagamoyo ni ushindani wa nani ata-host Eastern Hub kitu ambacho kitadhoofisha sana project ya Lamu.
 

Binafsi naamini kabisa wangeboresha bandari zetu za Dar,Tanga na Mtwara sambamba na kufufua njia ya reli ya kati na ile ya Tanga pamoja na TAZARA kama ingewezekana tungeona mabadiliko makubwa sana. Tatizo la hii nchi yetu ni pale watawala walipoamua kwa makusudi na kwa masilahi yao binafsi kuwafunika ama kutothamini ushauri wa wataalamu na kuendesha nchi jinsi wanavyofikiri wao na kushauriwa na marafiki/ndugu zao.
 


"China inapotoa mkopo, kuweka sharti kwa mkopaji na kutoa kitu kitakachoinusha na kutoa
Mfano wa nchi ya Angola, ambayo ilipewa mkopo kwa sharti la kupatiwa visima vya gesi, hivyo ni lazima Serikali ya Tanzania imetoa sehemu ya maliasili zake kwa mkopo huo"

Zitto Kabwe Gazetti la Rai
Imeandikwa na Na Charles Mullinda
Alhamisi, Januari 17, 2013 06:16
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…