Witness from the front line: Hili zoezi la sensa mlioko juu msiporekebisha haya kwa haraka tegemeeni taarifa mbovu kuwahi kutokea

Ni kuchoshana tu, nilivyoona semina siku 21 nikajiuliza ni sensa gani hii kumbe muendelezo wa kuborobga kwao.
 
Mnatumia GPS ya kwenye simu au hizi Garmin GPS? Sijui mfumo mnaotumia lakini mimi nimeshiriki mara kadhaa kwenye zoezi la sensa ya miti msituni (forest inventory) kwa kutumia mfumo huo unaosema ambapo makarani wetu (wanavijiji) tuliwafundisha mambo yafuatayo

1.Matumizi ya smartphone ambayo imepakiwa program yenye dodoso la kuhesabia miti

2. Matumizi ya GPS ndogo ambayo iko connected na smartphone kwa blue tooth. Hii GPS inafanana na power bank ndogo na mtumiaji anaiwasha na kui connect na smartphone halafu anaiweka mfukoni.

3.Power bank mbili zenye uwezo mkubwa kwa ajili ya kuchaji simu na GPS mkiwa field. Tulitumia only one week kuwa train Hawa wanakijiji na kufanya mazoezi kwa siku mbili kabla ya kwenda msituni for actual exercise.

Baada ya hapo waliweza kwenda msituni kwenye plots maalum na wakifika kwenye plot husika anasimama center ya plot na kupima miti yote iliyoko kwenye hiyo plot. Mfano wa data anazoingiza kwenye dodoso ni : Jina la msitu, Kijiji, kata, Tarafa, wilaya, Mkoa, namba ya plot, plot size, hali ya msitu ulivyo kwenye hicho kiplot, vegetation types, kama Kuna uharibifu (moto, kilimo, miti imekatwa etc).

Data nyingine ni jina la mti, unene/kiuno cha mti, urefu wa miti 3 kwenye plot, idadi ya visiki vilivyopo na unene wake etc.. Ukumbuke kwamba dodoso limetengenezwa kukuongoza kuchukua data systematically kuanzia juu kwenye jina la msitu mpaka kwenye plot namba na mengineyo, ukiruka step huwezi kwenda hatua inayofuata maana entry inagoma. Kuna hatua ya kuchukua coordinates za plot, pia kuna hatua ya kupiga picha ya hicho kiplot. Mwisho kabisa inakuletea option ya kuedit and then SAVE.

Kama eneo la msitu ulipo kuna network hilo faili ulilosevu unaweza kulituma kwenda kwenye server iliyoko ofisini. Kama hakuna network pia haina shida, plot moja ikiisha na kuwa served kwenye simu, dodoso linaenda kwenye new page unaanza tena na plot ya 2,3,4 etc..mpaka hata plot 500.

Ninachotaka kusema ni kwamba kwa technology ya sasa ilipofikia ilitakiwa hilo zoezi liwe rahisi sanaaaaa... All in all pole sana... Hivi wanawapa nauli za bodaboda au baiskeli ya kukodi au ndiyo mguu kwa mguu? Maana vijijini nyumba ziko mbalimbali...
 
CCM wanataka Sensa ya kuombea fedha za kusomesha watoto wao Jana SHAKA amesema samia tutamchagua mpaka achoke mwenyewe Sasa Unategemea nini kwenye hiyo Sensa !
Wanazi wa Magufuri wakati ule wakisema atakuwa Rais mpaka afie pale mkawaona ni kunguni, leo shaka anaongea yale yale mnakenua aseee!!.
 
Kama lile zoezi dogo tu la kuandika vibao vya anuani ya makazi walilipua, hiyo ya sensa inayohusisha mpaka GPS naona ndio wataparua kabisa.

Japo sioni sababu kwanini huyo muhusika wa sensa arudi kwenye eneo la kuchukua data endapo hiyo GPS itafeli kama tayari data za eneo husika atakuwa nazo, kwanini asijaze tu maisha yaendelee..
 
Bwana karani pambaneni kujaza mitaarifa ya uongo idadi ya watu isome 140million ili kumuhenzi mzee wetu aliyekuwa akihubiri injili ya kufyatua watoto kama tofali
 
Hao IT wako wenyewe hawaelewi hata hicho ulichogundua wewe ndio maana wanakua wakali
Shida ndio inaanzia hapo, mleta mada yeye amegundua tatizo la mfumo na anahitaji ufanyiwe marekebisho ila inategemea na huo mfumo umetengenezwa vipi? Shida ndio inaanzia hapo maana ili kufanya marekebisho kwa mujibu wa maelezo yake na nilivyomuelewa huo mfumo unabidi ufumuliwe tena upya uanze kufumwa upya kisha ufanyiwe marekebisho kwenye baadhi ya taratibu za mfumo, swali ni moja tu huo mfumo umetengenezwa from scratch na IT wa hapa hapa bongo au umetengenezwa na IT wa nje ya nchi (umenunuliwa kutoka nje ya nchi)?
 
Hongerq sana mzalendo.
Yamkini umeuelewa mfumo huo kwa haraka sana na madhaifu yake. Kati ya sehemu ya kumulikwa haraka ni mfumo huo vinginevyo zoezi zima litachukua muda mrefu sana na lisiwe na majibu.
Serikali yetu ni sikivu, nina imani wataliona hili
 
Hawatakusikiliza coz wanakazana kulamba keki ya sensa huku makarani wakipewa wali maharage yanayonuka.

Kuna sehemu wamelipwa sh 200,000 tu siku ya 15 leo huku wakilala guest houses na kujtegemea chakula cha jioni.

Kile kibibi kinasisitiza eti uzalendo mbele. Hawajui magumu tupatayo wala roho ya huruma kale kabibi hakana.

Hapa ni punda afe mzigo ufike. Mzigo utafikaje wakati punda kafa?
 
Mkuu hii nchi ngumu Sana , Bora hata mfumo mlioutumia , upo simple , na friendly , huu mfumo wa CS entry actually not bad in such , but kuna error hyo ya GPS kusoma nje ya eneo ulilopo , wanacommand kutotafta majira nukta ukiwa chini ya mti, au ndani ya nyumba , hata kukiwa na poor visibility (atmospheric barrier ) unashangaa upo DSM majira nukta yanasoma Tanga ....

Shida inakuja kuna nyumba wanazengo wanaishi mstuni , ili utafte eneo la wazi kuchukua GPS inakulazumu uwe away kama Mita 800 hv kulipata eneo la wazi with clear sky ,...!! Yote Tisa kumi waweke option ya ku-ommit , GPS iliyoenda wrong badala ya kufuta kazi yote ....

Kama huko ofisi ya takwimu hawana IT proffessional , wawaite ma IT wa nje , badala ya zoezi Zima kwenda terrible wrong , Kwa kesi ndogo kama hyo , huku nchi inatumia multbillion Tsh
 
TATIZO LINGINE KUBWA LIPO KWA MAKARANI NA WAKUFUNZI, BAADHI YAO NI WEUPE PEEEE....!!

WAMEPEANA KAZI MWISHOWE INAENDA KUHARIBIKA.

WAMEKUJA MTAANI KWANGU KWENYE MAJARIBIO NI WEUPE AISEEE...
Mambo kama haya wawe wanaacha siasa , baadh ya wakufunzi Kwa kweli ni janga , huyu anakwambia ukiwa unatafuta majira nukta zungusha tablet , mwingine anakwambia inabd utulie usitingishike, mwingine anakwambia zima Kwanza location , mwingine anasema boost na internet , huyu anasema huruhusiwi kuwa na simu au kuweka laini kwenye tablet , yaan ni vurugu tupu sa sjui hyo internet unaipataje
 
Mimi pamoja na Babe wangu wa JF Sky Eclat tumeipenda sana hiyo picha ya 'Kaya'😁😁😁
Mkuu hyo Kaya ina wanakaya 30 , maswali Kwa kila mwanakaya ni Kati ya 70-100 kulingana na umri , jinsia na shughuli za kiuchumi , na ili upate data Kwa Usahihi hapo itakulazimu ukae masaa si chini ya matatu mpak ma nne , na hap umekabidhiwa kitongoji kizima na sku za kuhesabu ni sita tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…