Hii habari mbona siielewi? Nini hasa kilichotokea? Walipigana au Sofia ndiye aliyempiga mwenzie? Tunaposema hadharani tuna maana gani? Nilidhani haya yalitokea kwenye kikao cha ndani na si kwenye public forum? Hiyo kauli chafu ilitokana na nini? Na ni nini hasa kilisemwa?
Ha ha haaaaa. Inabidi ufanye extracurricular independent study kujua kilichojiri kwenye tukio lolote Bongo.
SOPHIA SIMBA
``Kikao chetu kilikuwa cha siri, wewe habari hizo umezipata wapi? Mimi ni kiongozi makini, najua ninachokifanya, siwezi kutoa siri ya kikao, labda umfuate huyo aliyekuambia,``
``Wewe sijui leo ni mtu wa ngapi kunipigia simu, watu wengi wamenipigia eti wanauliza kulikuwa na masumbwi kati yangu na Janeth. Sasa kwa nini mnaniuliza, huyo aliyeamua kuvujisha siri za kikao basi na awamalizie kilichoendelea,``
``Kama anakwenda kushitaki anayo haki ya kufanya hivyo, akashitaki tu,``
``Namimi pia nina malalamiko kwake, mengi sana tena mazito, hata mimi nitamshitaki,``
JANETH KAHAMA, Mwenyekiti UWT, Mkoa
``Alitaka kunidhuru, nilikuwa katika wakati mgumu, maana hata wanaume na nguvu zao walipomshika asije kuniumiza, bado aliwasukumiza,``
``Katika hali hiyo huwezi kukumbuka jina wala sura ya mtu, nilichokumbuka mimi ni msalaba,`` alisema alipoulizwa kama anawakumbuka wajumbe waliomuokoa...alichokumbuka ni kukimbilia msalabani na kufanya maombi na kukemea roho ya ugomvi.
``Bi. Sofia ni kiongozi mkubwa sana na tunamheshimu, hivyo suala hili (la kudaiwa kupigwa naye) sijaenda kuliripoti polisi, bali nimeufikisha ugomvi huo katika vikao vya chama changu kwa kufuata taratibu na kanuni zilizopo... ninaamini huko kutatolewa maamuzi sahihi,``
``Nampenda sana Sophia, sina kinyongo naye,``
``Siwezi kumlaumu wala kusema barabarani kama alivyosema, mimi nitamfikisha kwenye vikao vya maadili, ndivyo taratibu zetu zinavyosema,``
``CCM hakuna jela, kwamba nikimpeleka huko atafungwa, lengo nikuhakikisha anapata nafasi ya kutoa madai yake,`` alisema. Hata hivyo, alikana kumhujumu Sophia kwa kutomwalika kwenye vikao vya UWT kama ilivyodaiwa.
WAJUMBE WALIOSHUHUDIA NA WAPAMBE WENGINE WENGINE
Anna Abdallah, Mwenyekiti UWT, Taifa
``Kwanza mimi siko Dar es Salaam, niko Dodoma, lakini pia si mjumbe wa kikao hicho. Hayo mambo yetu ya kuokoteza mitaani, msiniulize mimi,
Ninachojua, kesho tuna kikao cha Baraza Kuu, lakini habari ya nani na nani wamegombana, sitaki kuyajibu,``
John Guninita (Mwenyekiti wa CCM, Mkoa)
``Unajua Waziri Simba alitoa malalamiko yake kwangu wakati mkutano wetu tayari ukiwa umemalizika, hapakuwa na ugomvi mkubwa kama unavyouliza, bali Mwenyekiti wa UWT Mkoa (Kahama) alikuwa akijaribu kutoa ufafanuzi,``
Jina Limehifadhiwa na Chanzo Chetu (Mwenyekiti na Katibu wa Taifa, Chama cha Wadaku wasiojulikana!)
``Usifikiri uwaziri wako na kupata ofisi pale Ikulu vitakusaidia, huu ni uchaguzi wa Chama, heshimu taratibu za chama,`` chanzo chetu kilimnukuu Kahama.
``Wakati Waziri Simba akiendelea kusema, Mama Kahama alisimama na kuanza kusema: Sijakutukana, sijakutukana, hizi nafasi ni za Mungu, kwanini tuvunjiane heshima,`` alisema huku akisimama kuelekea alipokaa Mama Sofia.
``Kuona hivyo, wajumbe tuliamua kuingilia kati kwa kuwashika, huku wengine wakimsaidia Mama Kahama, kwani alikuwa amepandisha presha,``
Inasemekana habari ndio hiyo!