Wito butu wa mgomo kufuatia ripoti ya CAG

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Ni vigumu wito wa kiongozi wa chama kutenganishwa na chama:

Screenshot_20230411-202721.jpg

Ingekuwa vyema tukapeana uthibitisho ili japo kujua tunaposimama.

"Ikumbukwe kodi za kufikia nusu ya kwanza ya mwaka huu zilikwisha lipwa kufikia 31/3/2023."

Hivyo:

1. Wito huu unategemewa kutekelezwa vipi?

2. Kwanini vyama hivi haviko tayari kuwapo bega kwa bega kwenye mapambano yenye tija?

3. Hivi ndivyo Raila au walivyokuwa wakifanya kina Slaa au Maalimu Seif?

4. Tumepotea maboya kiasi hiki?

Niwaombe viongozi wetu kujitafajari. Kama vipi tuwe na viongozi walio tayari kwa mapambano kweli kweli.

"Watu hao mbona wapo wengi tu?"

Bila hivyo na kwa mwendo huu hakuna mtu kwenye ripoti ya CAG ataachia ngazi wala nini.

Labda kama tumeanua kuwa wasanii kama shishi tu.
 
🤩🤩🤩 Boniyai!

Makamanda uchwara utawaona hapa sasa. Yaani ni mwendo wa kupita juu kwa juu. Kama hawaoni vile.

Wanasubiri wajue upepo utaelekea wapi ndipo wachomoze japo pua zao nje.

Wanaona heri kusubiri hisani za mama badala ya kuona fahari kuzitumia funguo zote walizo nazo mikononi kupata wanavyostahili.

Ushauri wa bure, makamanda kama hao wangejipanga kustaafu tu.
 
Hawa jamaa wakiendewa kwa style hii ndio tutaelewana.

Kama pesa zinapigwa na kila mmoja haziingizwi kwenye mfumo, sioni haja ya kulipa huo ushuru na vinginevyo, tunachezeana tu.

Kama tuliruhusiwa kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake, wenzetu wameshajiongeza, wengine tunasubiri kitu gani? basi na kila mmoja ale kwa kutumia akili yake.
 
🤩🤩🤩
 
Vita vya ukombozi havipiganwi hivi ndugu zangu. Vita vya ukombozi havipiganwi kwa kuwa set watu kupigana mmoja mmoja kivyake vyake huko aliko. Umoja ni nguvu:

Labda kama ni kujaribu kujitoa kimaso mason tu au kuweka mazingira ya mtu kujichumia janga peke yake na kula na wa kwao.

"Kwamba watu wasipoitikia wito butu kama huu tuseme watanzania ni wajinga hawakuunga mkono kama asemavyo Pascal Mayalla ?"

Vita vya ukombozi hupiganwa pamoja. Ndiyo maana vishindo vya wakoma viliwakimbiza washami.

Vita vInavyoitishwa namna hii vina tofauti gani na miito ya binadamu aliye ndani ya nyumba kumtaka mbwa nje huko amkamate mwizi?

Raila hapigani hivi kumfukisha Gachagua kutepeta namna hii:

Screenshot_20230403-204008.jpg

Alipo huyo ana tofauti gani na huyu hapa?

FtGW0sQX0AA8O-q.jpeg

Kama hii ndiyo iliyo miito yetu iliyo thabiti kabisa ya ukombozi, pana haja ya kurudi kwenye drawing board kuyaangulia tena malengo yetu, watu wetu na viongozi wetu. Muhimu kujitidhisha kama tuko mahali sahihi na kwenye njia sahihi. Yawezekana malengo yamebadilika.

Ni heri tukawa wazi nini tunataka badala ya kujidanganya au kutokuwa na dira wala mwelekeo.
 
Vita vya ukombozi havipiganwi hivi ndugu zangu. Vita vya ukombozi havipiganwi kwa kuwa set watu kupigana mmoja mmoja kivyake vyake huko aliko. Umoja ni nguvu:

Labda kama ni kujaribu kujitoa kimaso mason tu au kuweka mazingira ya mtu kujichumia janga peke yake na kula na wa kwao.

"Kwamba watu wasipoitikia wito butu kama huu tuseme watanzania ni wajinga hawakuunga mkono kama asemavyo Pascal Mayalla ?"

Vita vya ukombozi hupiganwa pamoja. Ndiyo maana vishindo vya wakoma viliwakimbiza washami.

Vita vInavyoitishwa namna hii vina tofauti gani na miito ya binadamu aliye ndani ya nyumba kumtaka mbwa nje huko amkamate mwizi?

Raila hapigani hivi kumfukisha Gachagua kutepeta namna hii:

View attachment 2584947

Alipo huyo anatofauti gani na huyu hapa?

View attachment 2584948

Kama hii ndiyo iliyo miito yetu iliyo thabiti kabisa ya ukombozi, pana haja ya kurudi kwenye drawing board kuyaangulia tena malengo yetu, watu wetu na viongozi wetu. Muhimu kujitidhisha kama tuko mahali sahihi na kwenye njia sahihi. Yawezekana malengo yamebadilika.

Nu heri tukawa wazi nini tunataka badala ya kujidanganya au kutokuwa na dira wala mwelekeo.
Tatizo unachanganya mazingira, na usituweke kundi moja na wakenya, wale jamaa wanajielewa hawana uoga huu tuliona nao sisi.

Huyo Jacob alichosema hapo namuunga mkono kwa asilimia 100%, kwasababu amemuachia kila mmoja wetu jukumu la kujiongeza kivyake pale alipo.

Inawezekana atakuwa amefanya hivyo makusudi akijua fika sisi ni makondoo, kwani wameshajaribu kututaka tufanye hicho utakacho bahati mbaya hakuna mmoja wetu aliyejitokeza kuwaunga mkono.

Nashangaa sijui kwanini unaendelea kuamini tatizo letu ni viongozi wetu na sio ukondoo wetu?!
 
I think lengo ni kujenga public awareness. Sio wazo BAYA ila ni suala ambalo linahitaji utulivu. Sio dhambi
 
Shida za nchi yetu huwezi kulinganisha na za wakenya hata siku moja nataka uelewe hivyo bwana mdogo!
Mtanzania atalia njaa kwa sababu kakosa pesa ya kwenda kunywa pombe au soda, mkenya akilia njaa ni hakuna pesa ya kunua chakula hata cha siku hiyo mmoja, na hata ukipata hamna hicho chakula!
Kenya haina pesa za kulipa watu mshahara [emoji2959]
Wewe acha hiyo kabisa!
Watanzania sio waoga wala wajinga bali hawana shida muhimu ya kuwapeleka barabarani!
Labda kwenu ndio kwenye wehu!
Upinzani wenyewe ndio huu?
Wacha hiyo kabisa walahi [emoji2959]
035ce4d3-e4b6-4b6a-958b-1aebf5630071.jpg
 
Tatizo unachanganya mazingira, na usituweke kundi moja na wakenya, wale jamaa wanajielewa hawana uoga huu tuliona nao sisi.

Huyo Jacob alichosema hapo namuunga mkono kwa asilimia 100%, kwasababu amemuachia kila mmoja wetu jukumu la kujiongeza kivyake pale alipo.

Inawezekana atakuwa amefanya hivyo makusudi akijua fika sisi ni makondoo, kwani wameshajaribu kututaka tufanye hicho utakacho bahati mbaya hakuna mmoja wetu aliyejitokeza kuwaunga mkono.

Nashangaa sijui kwanini unaendelea kuamini tatizo letu ni viongozi wetu na sio ukondoo wetu?!

Hakuna mazingira yanayochanganywa hapa. Kwamba wakenya wanajitambua kuliko sisi sote hayo yatakuwa matusi (akiyaita Mwinyi ya nguoni) kwa watanzania.

Wameacha lini watanzania kujitambua? Baada ya kina Nyerere, Slaa, Mtikila, Maalim Seif na wa namna hiyo kutundika daruga ukutani?

Ninaamini unafahamu ni kwa kujizuia kiasi gani tunajaribu kuweka mawazo yetu ya dhati hadharani salama katikati ya macho ya mamba na fisi.

Hudhani kuwa ilikuwa muafaka kwamba:

1. Tukafahamishana kwa wazi kabisa malengo yetu hasa ni nini, labda tukaweka hata na tarehe ya nini tukitegemee lini ikiwezekana?
2. Tukapeana action plan ya nani anafanya nini ili tuweze kutathimiana kulingana na malengo yaliyopo?
3. Kwamba nafasi za uongozi zikawa kulingana na ahadi za mtu kutufikisha kwenye malengo tuliyokubaliana?
4. Kwamba kushindwa kuyafikia malengo au kutokuwa na sababu za msingi za kushindwa, kuwa ni sababu tosha ya awaye yote kuwajibika?
5. Nk.

Si kuwa tuna matatizo kwenye dira na mwelekeo?

Ikumbukwe:

1. Kutofautiana kimawazo ni jambo la afya.
2. Uongozi sI fursa
3. Uongozi una wajibu.
4. Uongozi ni kwa mujibu wa sera na agenda.
5. Ukombozi ni pamoja na risks zake kama zilivyo kwa kila mmoja wetu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Shida za nchi yetu huwezi kulinganisha na za wakenya hata siku moja nataka uelewe hivyo bwana mdogo!
Mtanzania atalia njaa kwa sababu kakosa pesa ya kwenda kunywa pombe au soda, mkenya akilia njaa ni hakuna pesa ya kunua chakula hata cha siku hiyo mmoja, na hata ukipata hamna hicho chakula!
Kenya haina pesa za kulipa watu mshahara [emoji2959]
Wewe acha hiyo kabisa!
Watanzania sio waoga wala wajinga bali hawana shida muhimu ya kuwapeleka barabarani!
Labda kwenu ndio kwenye wehu!
Upinzani wenyewe ndio huu?
Wacha hiyo kabisa walahi [emoji2959]View attachment 2584996
Hao watanzania wanaolilia pesa za kwenda kunywa pombe uliwaona wapi, wakati huku mitaani kila siku mahitaji muhimu yanazidi kupanda bei?

Wakenya nao walikuwa wakiandamana kwasababu ya kupanda kwa gharama za maisha, hapo tofauti yetu na wakenya kwenye sababu ya kuandamana iko wapi?
 
Hakuna mazingira yanachanganywa hapa. Kwamba wakenya wanajitambua kuliko sisi sote hayo yatakuwa matusi (akiyaita Mwinyi ya nguoni) kwa watanzania.

Wameacha lini watanzania kujitambua? Baada ya kina Nyerere, Slaa, Mtikila, Maalim Seif na wa namna hiyo kutundika daruga ukutani?

Ninaamini unafahamu ni kwa kujizuia kiasi gani tunajaribu kuweka mawazo yetu ya dhati hadharani salama katikati ya macho ya mamba na fisi.

Hudhani kuwa ilikuwa muafaka kwamba:

1. Tukafahamishana kwa wazi kabisa malengo yetu hasa ni nini, labda tukaweka hata na tarehe ya nini tukitegemee lini ikiwezekana?
2. Tukapeana action plan ya nani anafanya nini ili tuweze kutathimiana kulingana na malengo yaliyopo?
3. Kwamba nafasi za uongozi zikawa kulingana na ahadi za mtu kutufikisha kwenye malengo tuliyokubaliana?
4. Kwamba kushindwa kuyafikia malengo au kutokuwa na sababu za msingi za kushindwa, kuwa ni sababu tosha ya awaye yote kuwajibika?
5. Nk.

Si kuwa tuna matatizo kwenye dira na mwelekeo?

Ikumbukwe:

1. Kutofautiana kimawazo ni jambo la afya.
2. Uongozi sI fursa
3. Uongozi una wajibu.
4. Uongozi ni kwa mujibu wa sera na agenda.
5. Ukombozi ni pamoja na risks zake kama zilivyo kwa kila mmoja wetu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Mazingira yetu na wakenya kwenye sababu ya kuandamana hayatofautiani, sasa mbona wao walikuwa barabarani lakini sisi tulilala nyumbani?

Unasema tatizo ni viongozi, mbona Lissu alishatuonesha njia lakini tukagoma kumfuata?

Kama ni suala la ku prove something, naamoni sasa ni zamu yetu watanzania ku prove tunaweza tukiamua, lakini sio viongozi wao walishatuongoza tukawafelisha.

Hata mfano wa maandamano yaliyofanikiwa unaonionesha hapa, ni wa level ya chini ngazi ya mkoa, hapo ndipo Dr. Slaa na viongozi wengine walifanikiwa, lakini bado sijawahi kuona maandamano yakifanikiwa kwa ngazi ya juu zaidi.
 
Ni vigumu wito wa kiongozi wa chama kutenganishwa na chama:

View attachment 2584747

Ingekuwa vyema tukapeana uthibitisho ili japo kujua tunaposimama.

"Ikumbukwe kodi za kufikia nusu ya kwanza ya mwaka huu zilikwisha lipwa kufikia 31/3/2023."

Hivyo:

1. Wito huu unategemewa kutekelezwa vipi?

2. Kwanini vyama hivi haviko tayari kuwapo bega kwa bega kwenye mapambano yenye tija?

3. Hivi ndivyo Raila au walivyokuwa wakifanya kina Slaa au Maalimu Seif?

4. Tumepotea maboya kiasi hiki?

Niwaombe viongozi wetu kujitafajari. Kama vipi tuwe na viongozi walio tayari kwa mapambano kweli kweli.

"Watu hao mbona wapo wengi tu?"

Bila hivyo na kwa mwendo huu hakuna mtu kwenye ripoti ya CAG ataachia ngazi wala nini.

Labda kama tumeanua kuwa wasanii kama shishi tu.
Naunga mkono hoja haiwezekani kila siku tunachangia akina mbarawa, makamba, Nape mabilion ya fedha
 
Shida za nchi yetu huwezi kulinganisha na za wakenya hata siku moja nataka uelewe hivyo bwana mdogo!
Mtanzania atalia njaa kwa sababu kakosa pesa ya kwenda kunywa pombe au soda, mkenya akilia njaa ni hakuna pesa ya kunua chakula hata cha siku hiyo mmoja, na hata ukipata hamna hicho chakula!
Kenya haina pesa za kulipa watu mshahara [emoji2959]
Wewe acha hiyo kabisa!
Watanzania sio waoga wala wajinga bali hawana shida muhimu ya kuwapeleka barabarani!
Labda kwenu ndio kwenye wehu!
Upinzani wenyewe ndio huu?
Wacha hiyo kabisa walahi [emoji2959]View attachment 2584996

Mtanzania?

1. Mtanzania hudhani yeye ndiye anayejua yote ila si mwingine.
2. Mtanzania hudhani wengine wote ni wajinga isipokuwa yeye.
3. Mtanzania hudhani yeye ni bora zaidi kimataifa kuliko wengine wote duniani.
4. Si ajabu mtanzania huyo kumwita mtu mwingine asiyemjua kuwa ni bwana mdogo. Kwamba yeye ni bwana mkubwa 🤣🤣
5. Kiufupi mtanzania ni mjuaji mno!
6. Chini ni mtanzania huyo kwenye ubora wake:

Fs2EWsZXwAAqdRU.jpeg

Screenshot_20230319-081205.jpg

Uko vizuri mjomba.

Huyo ni yule mtanzania mjinga!
 
Mazingira yetu na wakenya kwenye sababu ya kuandamana hayatofautiani, sasa mbona wao walikuwa barabarani lakini sisi tulilala nyumbani?

Unasema tatizo ni viongozi, mbona Lissu alishatuonesha njia lakini tukagoma kumfuata?

Kama ni suala la ku prove something, naamoni sasa ni zamu yetu watanzania ku prove tunaweza tukiamua, lakini sio viongozi wao walishatuongoza tukawafelisha.

Hata mfano wa maandamano yaliyofanikiwa unaonionesha hapa, ni wa level ya chini ngazi ya mkoa, hapo ndipo Dr. Slaa na viongozi wengine walifanikiwa, lakini bado sijawahi kuona maandamano yakifanikiwa kwa ngazi ya juu zaidi.

Mkuu labda iwe kujitia hamnazo tu. Yaani kujaribu kuukimbia ukweli. Kwa maneno mengine kuamua kujidanganya wenyewe.

Matatizo yetu na wakenya ni yale yale kwa nini hatuandamani ... ?

Jibu ni rahisi na ninaamini hata mama Samia, mambuzi wote, mimi, wewe na yule wanalijua vizuri sana:

"Raila Odinga (Baba) Kamanda wa vita yuko wapi?"

Nimekupa mifano kadhaa kuwa maandamano yenye hamasa ya kutosha ambayo yamewahi kuwepo hapa nchini. Kinondoni kwenye kadhia ya Aquiline, alipokuwapo Slaa, alipokuwapo Maalim Seif, nk. Maandamano kama hayo hayakuwa ya kitoto.

"Kwani maandamano ya Raila yanayoitikisa Kenya yana watu hata 2,000? Siyo Kenya yote inayo andamana."

Kutotambua harakati kama hizi,

hakuwezi kupewa jina jingine zaidi ya kuwa ni kutaka kutojitendea haki wenyewe kwa kiwango cha juu tena kilichopitiliza.

Tambua bila Raila, Kenya hakuna maandamano.

Kwamba hatukutokea kwenye shughuli za Lissu? Lissu huyu?

Ed7tAaTXYAAKmfy.jpeg

Wapi hatukutokeai? JKNIA #1 au Kiluvya na askofu Mwamakula?

Kama huko tulitokea unalenga kuonyesha wapi watu hatukutokea? Kama unadhani hatukutokea umejiridhisha na sababu zakutokutokea, zikiwamo kutokuwapo kwa malengo stahiki kama yalivyo kwenye wito huu?

"Nikuombe utuletee mrejesho baada ya wito huu wa mgomo."

Askofu Mwamakula aenda alipozuiliwa Lissu kumtia nguvu

Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi

Haitakuwa ajabu kama kamanda Lissu kokote aliko atakuwa anasikitika kutokana na maendeleo mapya haya.

Ninao uhakika kuwa kamanda Lissu ana ufahamu ushupavu wa vijana wake, ambao jiwe katika ubora wake alitepeta vilivyo.

Cc: Zawadini
 
I think lengo ni kujenga public awareness. Sio wazo BAYA ila ni suala ambalo linahitaji utulivu. Sio dhambi

Kutoa kitisho usichoweza kukitimiliza (fulfil) ni kosa kubwa la kiufundi (tactical mistake).
 
Hao watanzania wanaolilia pesa za kwenda kunywa pombe uliwaona wapi, wakati huku mitaani kila siku mahitaji muhimu yanazidi kupanda bei?

Wakenya nao walikuwa wakiandamana kwasababu ya kupanda kwa gharama za maisha, hapo tofauti yetu na wakenya kwenye sababu ya kuandamana iko wapi?

Raila Amolo Odinga (baba) angekuwa mtanzania, watanzania wangeandamana. Vivyo hivyo kama Julius Malema, Bobi Wine au Kizza Besigye kama wangekuwa watanzania.

BIla watu kama hao hata huko wanakoandamana leo wangekuwa wametepeta kama sisi tu.
 
Back
Top Bottom