denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Mjomba jaribu kutofautisha yale maandamano ya kwenda kumpokea Lissu, na maandamano haya unayotaka sasa ya kudai haki, yale ya kwenda kumpokea Lissu hayakuwa na tatizo lolote toka kwa vyombo vya ulinzi na usalama.Mkuu labda iwe kujitia hamnazo tu. Yaani kujaribu kuukimbia ukweli. Kwa maneno mengine kuamua kujidanganya wenyewe.
Matatizo yetu na wakenya ni yale yale kwa nini hatuandamani ... ?
Jibu ni rahisi na ninaamini hata mama Samia, mambuzi wote, mimi, wewe na yule wanalijua vizuri sana:
View attachment 2585358
"Raila Odinga (Baba) Kamanda wa vita yuko wapi?"
Nimekupa mifano kadhaa kuwa maandamano yenye hamasa ya kutosha ambayo yamewahi kuwepo hapa nchini. Kinondoni kwenye kadhia ya Aquiline, alipokuwapo Slaa, alipokuwapo Maalim Seif, nk. Maandamano kama hayo hayakuwa ya kitoto.
"Kwani maandamano ya Raila yanayoitikisa Kenya yana watu hata 2,000? Siyo Kenya yote inayo andamana."
Kutotambua harakati kama hizi,
View attachment 2585372
hakuwezi kupewa jina jingine zaidi ya kuwa ni kutaka kutojitendea haki wenyewe kwa kiwango cha juu tena kilichopitiliza.
Tambua bila Raila, Kenya hakuna maandamano.
Kwamba hatukutokea kwenye shughuli za Lissu? Lissu huyu?
View attachment 2585345
Wapi hatukutokeai? JKNIA #1 au Kiluvya na askofu Mwamakula?
Kama huko tulitokea unalenga kuonyesha wapi watu hatukutokea? Kama unadhani hatukutokea umejiridhisha na sababu zakutokutokea, zikiwamo kutokuwapo kwa malengo stahiki kama yalivyo kwenye wito huu?
"Nikuombe utuletee mrejesho baada ya wito huu wa mgomo."
Askofu Mwamakula aenda alipozuiliwa Lissu kumtia nguvu
KUMFUNGIA NI SAWA KABISA MAANA ALIKUWA ANAPOTOSHA RAIA KUWA JPJM AMEWAITA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KUPANGA NJAMA ZA KUHUJUMU UCHAGUZI. SASA UNAONA KAKUBALI KOSA LA KUSEMA UONGO. CHADEMA KUPITIA WAWAKILISHI WAKE KWENYE TUME YA MAADILI YA NEC WALIOMBA APUNGUZIWE ADHABU. WANGEACHA KUMFUNGIA...www.jamiiforums.com
Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi
Imekuwa kawaida kusikia watanzania wakiwaita watanzania wenzao kuwa ni waoga (cowards). Maajabu ya Mussa. Kwani hao wanaowaita wenzao kuwa cowards utaifa wao si ni huu huu au wao ni walamba asali? Uhalisia wa mambo ni kuwa wanaowaita hivyo wenzao, nia yao ni kutokuwepo mstari wa mbele...www.jamiiforums.com
Haitakuwa ajabu kama kamanda Lissu kokote aliko atakuwa anasikitika kutokana na maendeleo mapya haya.
Ninao uhakika kuwa kamanda Lissu ana ufahamu ushupavu wa vijana wake, ambao jiwe katika ubora wake alitepeta vilivyo.
Cc: Zawadini
Hata yale ya Aquilline [RIP] hayakuwa na vitisho kabla, yaliibuka ghafla tu ndio maana waandamanji ambao mwanzo walikuwa wamehudhuria tu mkutano wa siasa wakasonga, it was easy from that point of view..
Lakini maandamano ya kudai haki unajua nini kina Mambosasa walikuwa wakisema kabla kwa waandamanaji, ni vitisho tu, mfano mkitokea tutawavunja miguu!.
Ndio maana nasema na nitarudia tena kusema, wakenya wana ujasiri kuliko sisi, kwasababu wakati sisi tukiogopa vitisho vya kina Mambosasa, wao wanatishwa then wanasema wanataka kuionja tear gas ya 2023! kisha wanaingia barabarani..!! wakati sisi tukitishwa, Lissu haoni mtu, this is the fact wala sio kuukataa ukweli kama unavyosema.
Ndio maana hata hao vijana wa Lissu unaowazungumzia mimi sijui ni wapi, mbona hatukuwaona wakati ule Lissu aliposema akiibiwa kura hapatatosha? au hakuibiwa?!