Wito butu wa mgomo kufuatia ripoti ya CAG

Mjomba jaribu kutofautisha yale maandamano ya kwenda kumpokea Lissu, na maandamano haya unayotaka sasa ya kudai haki, yale ya kwenda kumpokea Lissu hayakuwa na tatizo lolote toka kwa vyombo vya ulinzi na usalama.

Hata yale ya Aquilline [RIP] hayakuwa na vitisho kabla, yaliibuka ghafla tu ndio maana waandamanji ambao mwanzo walikuwa wamehudhuria tu mkutano wa siasa wakasonga, it was easy from that point of view..

Lakini maandamano ya kudai haki unajua nini kina Mambosasa walikuwa wakisema kabla kwa waandamanaji, ni vitisho tu, mfano mkitokea tutawavunja miguu!.

Ndio maana nasema na nitarudia tena kusema, wakenya wana ujasiri kuliko sisi, kwasababu wakati sisi tukiogopa vitisho vya kina Mambosasa, wao wanatishwa then wanasema wanataka kuionja tear gas ya 2023! kisha wanaingia barabarani..!! wakati sisi tukitishwa, Lissu haoni mtu, this is the fact wala sio kuukataa ukweli kama unavyosema.

Ndio maana hata hao vijana wa Lissu unaowazungumzia mimi sijui ni wapi, mbona hatukuwaona wakati ule Lissu aliposema akiibiwa kura hapatatosha? au hakuibiwa?!
 

Mkuu kwenda kumpokea Lissu na Kiluvya enzi za aliyekuwa jiwe kweli kweli haikuwa cha mtoto.

Kumbuka Jiwe, Sirro na timu yao nzima ilisema tusiweke mguu JKNIA. Kukumbusha zaidi, katuni hIzi hazikuwa by accident:



Hata Kinondoni iliyoishia na kupoteza maisha ya mtu haikuwa ndondondo. Risasi za moto kinyama zilikuwa zikirushwa na mabazazi wale.

Zanzibar hii Maalim, waliokufa watu wengi, tukiambiwa kutokana na risasi za askari wa kukodiwa kutokea huko tunakochagizwa tuhamie:

Your browser is not able to display this video.


"BIla Raila Odinga wakenya wametepeta kama sisi tu mjomba."

Kwamba wanataka tear gas, hiyo ni kwa sababu ya uwepo wa shujaa Odinga.

Siyo siri watu kama kina Lissu wanalo bashasha (charisma) lenye kuwaakisi waungwana wa aina za akina Kyagilanyi au Malema.

Ikumbukwe charisma hupewa na Mungu na si kila mtu anaweza kuwa nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…