Wito: Kamati Kuu ya CCM ifunguliwe Mashitaka Mahakama Kuu kwa Kumteua Mgombea Urais aliyekosa Sifa 2015

Jk angeridhia makubaliano yake na Lowasa, Magu asingekuwa Raisi
Kwenye ccm hamna wakati ambao rais aliyepita anaweza kuweka rais ajae anaemtaka yeye. Hii alifanya Nyerere tu.
Unatakiwa useme kama Mungu asingetaka, siyo binadamu
 
Siyo watu wote ni wajinga kama wewe, kama hakuna maovu mbona Nyerere na Mkapa hawasemwi kwa maovu kama yeye?
Shida ni nyinyi wafanyabiashara au watoto wao au chadema ambao mlikabwa koo kwenye kulupa kodi na mambo mengine ya ajabu.
Nyinyi ndo mlisema mnataka rais mkali coz jk anacheka cheka tu. Hamna mnachoridhika nacho
 
Unamaanisha kama aliiba uchaguzi kwa hiyo hata Rais tuliyenae si halali? Maana alitokana na uchaguzi huo, ni hivyo?
Hayo ni ya kwako. Samia kaletwa na Mungu, na nchi iko salama mikononi mwake
 
Kichaa aliyemudu kuanzisha miradi mikubwa ya mkakati
Miradi mikubwa ya kimkakati ndiyo nini? Kwani hii Tanzania unayoiona imeanza mwaka 2015? Chukua muda na tumia akili "kama unazo" ili ujuwe kuanzia Nyerere 1961-85 nini kilifanyika. Angalia barabara za kuanzia Dar- Tunduma, TAZARA na uanzishaji mashirika ya umma zaidi ya 400 huku kuna umoja wa kitaifa na elimu bure. Nenda kamuangalie AH Mwinyi 1985-1995 uone alifanya nini kwenye kuleta soko huria, barabara za njia 2 Dar es Salaam na barabara za Arusha Segera

Halafu njoo kwa BW Mkapa uone Baba wa uchumi na miundombinu namna alivyoteremsha deni la taifa. Yeye ndiye aliyehakikisha barabara ya Kahama-Nzega- Singida-Dodoma inakamilika ili Watanzania wa Kagera wasipite Uganda na Kenya wanapokwenda makwao

Mwishowe njoo kwa JKikwete uone alivyomailizia kuunganisha mikoa yote kwa barabara za lami kasoro Tabora - Mbeya.

Hawa watangulizi walifanya mengi kuliko hayo ila hawakuwa watu wa masifa kwa sababu walijuwa ndiyo kazi yao.

Nyinyi wajinga akina Siddo mumeingia mtego wa propaganda zake kwa kuwa hamkuwa na akili ya kutafuta taarifa. Kujenga daraja au kununua ndege isiwe excuse ya kuua watu bila sababu
 
Asante kwa darasa muruwa .
 
Hii kesi inafunguliwa lini?
 
Unanikumbusha watu wanao ahirisha kufikiri,yaani kwa lugha rahisi kujitoa ufahamu,,(kujizima data), unyumbu Ndiyo linaeleweka vizuri
 
Leo Nimetonywa kuwa shida inayozikumba social security fund pamomoja na nhif ni yeye kuchukua mihela na kwenda kutapanya anakokujua

Imepelekea nhif, nssf zote kufa ndo maana unaona wahangaika na kikokotoo
Magufuli alikuwa na mambo ya ajabu ajabu sana
 
Waliomuweka wakamatwe haraka
 
Umeandika nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…