Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa". Makala ya Leo ni
wito kwa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira NEMC, Kuwapiga Faini Mgodi Kuhusu Uchafuzi wa Mazingira kwa Sumu, usiishie kwenye kuwapiga tuu fine tuu, bali wawafidie waathirika na kama sumu hiyo ni lethal, wapandishwe kizimbani!
Paskali
Naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa". Makala ya Leo ni
wito kwa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira NEMC, Kuwapiga Faini Mgodi Kuhusu Uchafuzi wa Mazingira kwa Sumu, usiishie kwenye kuwapiga tuu fine tuu, bali wawafidie waathirika na kama sumu hiyo ni lethal, wapandishwe kizimbani!
Wajameni hii fine Kwa mgodi wa Barrick, japo ni adhabu kwa upande mmoja, ni majanga kwa upande mwingine na pia kuna fursa kama ilivyo kwenye kufa kufaana..Mgodi wa Barrick North Mara uliopo mkoani Mara umepigwa faini ya shilingi Bilioni moja na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kosa la uchafuzi wa mazingira baada ya bomba linalopitisha maji taka kutoka kwenye mgodi huo kupasuka na kutiririsha maji katika Mto Tigite unaomwaga maji yake Mto Mara.
Source: ITV
- Kupasuka Kwa bomba ni ajali kama ajali nyingine yoyote, lakini mgodi unapewa adhabu tuu kwasababu maji hayo yana sumu. Hivyo Barrick Wana suffer a double tragedy, wamepasukiwa bomba kutawagharimu kulikarabati na kugharimika kulipa faini.
- Kwa mujibu wa sheria zetu hao Barrick wakiisha karabati bomba Lao, na kuilipa hiyo fine, they are done and life goes as usual.
- It should not end up there, ilibidi utafiti wa kina ufanyike kujua madhara ya muda mfupi, muda wa Kati na muda mrefu wa athari za sumu hiyo, na Barrick wawajibike kufidia.
- Mfano kwenye madhara ya muda mfupi, inaweza kukutikana samaki wa mto Tigite na mto Mara baada ya kuingia sumu hiyo, sasa samaki hao sio salama kwa mlo, hivyo wavuwi wataathirika, wanapaswa kufidiwa.
- Wananchi wote wanaotumia maji ya mto Tigite na mto Mara wanaweza kuzuiwa kutumia maji hayo, wataathirika, wanahitaji kufidiwa.
- Wananchi waliotegemea kitoweo cha samaki mto Tigite na mto Mara wataathirika Kwa kukosa kitoweo, itabidi wafidiwe Kwa kununuliwa nyama Kwa siku za week days na kuku on weekends hadi sumu iishe na na samaki waanze kuvuliwa tena.
- Nemc wao watapiga pesa, sijaangalia sheria ya retention, ila pia fedha hizo ziwe righ fenced ili kufidia baadhi ya madhara.
- Wanasheria wetu wa Tanzania, nanyi msilale, maana wanasheria wetu huwa wamelala mpaka basi!. Kwa wanasheria wa nchi za wenzetu, faini hii ni fursa. Nendeni naeneo hayo, tafuteni watu walioathiriwa na sumu ya mgodi huo, wasainisheni kuwatetea pro borno, fungueni kesi za madai ya fidia Kwa waathirika mtapiga pesa!
- Taasisi za utafiti fanyeni utafiti wa athari za sumu hiyo kwa wananchi na conclusion iwe athari za sumu hiyo has claimed so many lives kiasa kwamba mna recommends, kuliko maisha ya watu kuathirika bora mgodi ufungwe!. Research hiyo ipite kwanza Barrick for their imput kabla haijawalishwa serikalini.. mtavuta.
- Kundi la mwisho, ni letu sisi media, tuandae IJ proposal za faida na hasara za migodi ya Barrick Kwa Tanzania, tui present for funding tutavuta
Paskali