Huko ulimwenguni wameshatabiri kuwa bei ya mafuta itazidi kupaa hadi 2045, kama hamuelewi maana ya mwendo kasi mtaielewa, ile ya kauli ya piga tajame TZ haifai kutumika tena.
Serikali kama inavyofukua madini basi sasa wakati umefika wa kuivuta juu hazina ya mafuta, na kwa vile kiwanda cha kusafishia mafuta kipo mbona kazi itakuwa rahisi.
Tusitegemee mafuta ya Uganda kwani mtegemea cha ndugu tunasema hufa masikini.
Serikali ya CCM ambayo ipo madarakani fanyeni hima juu chini hii sera muitangaze ingawa ACT wameshaanza kuhubiri, siku wakiitwaa serikali ya Zanzibar basi hawana simile na uchimbaji wa kuyavuta mafuta na si kuyatafuta tena kwani yapo yamejaa na inasemwa huko Pemba misitu inakauka kwa vuke la mafuta, kama Sultani wa Zanzibar alisema anawaachia vizazi basi sasa vizazi vipo tayari.
Msingojee siku mnaaza kuchimba watu duniani hawatumii tena injini za mafuta wanatumia umeme na tayari hybrid zimeanza kwa kasi huko ulimwenguni.
Msije kusema sikuwakumbusha - Mwiba.