Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Bila kumung'unya maneno naanza moja kwa moja kuwaasa wananchi wa Tanzania kulinda afya zenu wenyewe , hii ni kwa sababu usalama wa maisha yako ni HAKI YA KIKATIBA , mtu mdogo kama Meya wa Manispaa yoyote ile aliyetokana na udiwani wa kata hana mamlaka yoyote ya kisheria ya kuamuru mtu yeyote ahatarishe maisha yake ili awafurahishe viongozi wake .
Wala hakuna mtu yeyote mwingine mwenye cheo chochote kile kwenye nchi hii aliyeruhusiwa na KATIBA YA NCHI kuhatarisha maisha ya raia yeyote kwa sababu zozote zile , hivyo basi wananchi wote mnapaswa kupinga kwa nguvu zote hujuma zozote dhidi ya Uhai wenu kutoka kwa mtu yeyote mwenye cheo chochote , wala msione aibu kupigania kanuni bora za afya za kujikinga na maradhi ya mlipuko au maradhi mengine yeyote , kwa sababu HAKI YENU YA KUISHI MLIYOPEWA NA MUNGU inalindwa na Katiba ya nchi .
Naomba kuwasilisha .