Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,251
- 22,929
Ni miaka 63 sasa CCM ipo madarakani. Kimsingi hakuna maendeleo ya maana CCM iliyotuletea, isipokuwa bla bla nyingi miaka nenda miaka rudi na kuturudisha nyuma kimaendeleo miongo kadhaa.
Kila serikali iliyoingia madarakani ilileta usanii wa kisiasa na kiuchumi ule ule.CCM wanayosifia kwamba ni maendeleo si chochote kabisa ukilinganisha na rasilimali nyingi tulizo nazo na muda mrefu waliokaa madarakani. Tuamke Watanzania.After all hii ya sasa sio CCM,ila ni kikundi Cha watu wachache walioiteka CCM na serikali yake.
Comrade Magufuli katika awamu yake moja alijitahitahidi kubadilisha taswira ya Tanzania kwa kutuletea maendeleo kiasi fulani, lakini kwa bahati mbaya malengo yake na juhudi zake zilifishwa prematurely, inasikitisha sana.
Kwa jinsi hali ya kisiasa ilivyo nchini kwetu, hatuna jinsi yeyote ambayo kama Watanzania tunaweza kujinasua kwenye mkwamo wa kimaendeleo na kisiasa tulio nao sasa.Katiba haiheshimiwi kabisa na sioni uwezekano wa Bunge au hata wana siasa kutusaidia.Ingawa Bunge kwa kutumia katiba tuliyo nayo,kama lingekuwa bunge imara lingeweza kututoa kwenye mkwamo huu.Burkina Faso,Niger na Mali na sasa hata Botswana wanajikwamua,sisi tunashindwa wapi?Jibu ni kwamba tunaweza,hakuna tu utashi wa kisiasa.
Mwito wangu kama Mtanzania kwa Watanzania wenzangu ni huu, kama mpaka 2025 tusipopata Katiba mpya, na Tume Huru ya Uchaguzi, siku ya uchaguzi wote tubaki nyumbani tusiende kupiga kura.Naamini hii ndiyo lugha pekee CCM watakayoelewa.Sisi wananchi ndio tunaowapa wanasiasa legitimacy ya kutawala.Sasa kama wasipotupa Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi tubaki nyumbani,simply tuwanyime legitimacy ya kututawala.It is now or never, naomba tushirikiane wote.
NB: Please share this message widely from now to election day in 2025