Wayne
JF-Expert Member
- May 27, 2009
- 659
- 204
Tusijipe moyo kwa kufumbia macho MATATIZO ya msingi ya soka letu:Mi nafikiri tatizo letu( watanzania washabiki wa soka) kubwa ni kukosa subira.Tunataka mambo makubwa bila kuyatolea jasho (tazama DECI). Hivi wale vijana waliocheza jana tulitaka wafanye nini zaidi ya kufunga yale magoli mawili? Ni mafanikio makubwa sana kwao kuwafunga mabingwa wa bara la Oceania, tusitafute visingizio vya hali ya hewa n.k, tungefungwa sisi hakuna mtu amabaye angetaka kusikia visingizio vya timu haina uzoefu n.k
Hitimisho:
1. Ushindi amabao timu yetu imekuwa inaupata chini ya Maximo,hauondoi ukweli kuwa bado tuko safarini kuelekea mafanikio endelevu ya kisoka.
2. Tujiamini kuwa tunaweza, tuwape muda wachezaji, makocha n'k kuendelea kunoa wachezaji.
3. Watakaokuja kuiletea sifa nchi yetu ni vijana (under 17) wanaolelewa vizuri katika mafunzo ya soka ya kisasa, tuweke kipaumbele huko.
4. Vilabu ndio kisima cha kutoa wachezaji bora kwa timu ya taifa. Ziwekeze katika timu za vijana na kuajiri makocha bora.
1.Football Administration yetu ina matatizo megi na YAKUJITAKIA.Kuna WATU PALE TFF wamefanya TFF ni mali yao.Alizungumza Mogella kuhusiana na aina ya Viongozi waliopo pale kwa misingi ya kwamba wao wanaelimu.Elimu ni muhimu lakini unatakiwa upate na ukaribishe mawazo ya watu kama Mogella waliocheza mpira WAKAWEKA alama mpaka leo vizazi vinawakumbuka.Kayuni na wenzake wanaharibu kitengo kile cha Ufindi.
2.Uwezo wa wachezaji wetu TUNAOWAONA PALE uwanjani ni mdogo mno.Wachezaji TUNAOLETEWA timu ya taifa siyo BEST PLAYERS(tofautisha majina na uwezo) wengi wanaMAKUBALIANO MAALUMU na viongozi wa kitengo cha Ufundi TFF.
3.U-17 imemkimbiza TINOCCO ,mfano pale karume Tinocco alichagua wachezaji kwa kuwatambua kwa namba za jezi zao, siku ya kambi aliletewa vijana tofauti na kamati ya ufundi ya TFF,bahati nzuri alishtuka akauliza baadhi yao ambao walikuwa na features tofauti na wenzao, akajua ameingizwa mjini.Vilevile tusisahau kuwa muda wote alikuwa akitumiwa na Maximo timu ya taifa kama assistant wake baada ya Itamar kuondoka,sisi wengine hatukushangaa alipoondokea kulekule Abdijan.
4.Maximo amepewa mkataba mpya wa kufundisha,lakini bado anahangaika na kujenga kikosi UKITAKA KUJUA UWEZO WA MAXIMO nenda kazungumze na ITAMAR pale Azam ndipo utakapojua kuwa WaZT tumeingia mkenge,juzi Mtemi Ramadhani kaonyesha concern yake pia kwa suala ya kufumua kikosi mara kwa mara.Kimsingi tunahitaji KOCHA MPYA badala ya Maximo huwezi kuwa mtu usiye na MSAMAHA,hakuna ASIYEJUA UWEZO WA BOBAN ,he is the best midfielder kwa sasa nchini kwetu,GAGARINO alikuwa mtovu wa nidhamu lakini mwisho wa siku tulikuwa tunampima kwa results.
5.Administration ya Vilabu ni UTAPELI MTUPU.Nini amefanya MANJI/MADEGA pale jangwani? HAKUNA, jengo lilelile la mwaka 47 vilevile kwa watani wao Simba hakuna maendeleo,kina MAGORI na wenzake FRIENDS OF SIMBA hakuna kitu ambacho wanaweza kuonyesha wakajivunia wamefanya ambacho ni life yake ni zaidi ya miaka 10 or 20 ijayo.TUNASHAWISHIKA KUSEMA WOTE HAO SIO WAFADHILI WA HIVI VILABU bali WANAVITUMIA KUFANIKISHA MALENGO YAO.Hapa tunaona kumbe hata wazee wale wazamani wanaonekana walikuwa na Vision nzuri kuliko wa sasa,ZIPO WAPI SIMBA B na YANGA B, kule kulitoa wachezaji wazuri,Michezo mashuleni hoi,VIWANJA VYA MICHEZO VINAUZWA KWA WAWEKEZAJI.
6.Chama cha Waamuzi kiache kuendeshwa kiubabaishaji,ndiyo maana hatuna hata mwamuzi mmoja anayechezesha hata mashindano makubwa ya Afrika.Tangu waondoke kina Hafidh Ally imekuwa aibu tupu.Jana goli la kwanza lilikuwa offside ya wazi Mwamuzi alitubeba ni fedheha.
6.Tushangilie ushindi lakini TUACHE UNAZI,tunashabikia hata kile kisichofaa.