Wito wa Gen Z wa Kenya kwa vijana wa Afrika

Wito wa Gen Z wa Kenya kwa vijana wa Afrika

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Anaitwa Julius! Ni Gen Z kutoka nchini Kenya.

Amewaasa vijana wa Afrika kuwa njia pekee ya kuleta MAGEUZI ni kupinga maovu yanayofanywa na Serikali zao. Katoa wito huo alipokuwa mahakamani kwa tuhuma za kusababisha uvunjifu wa amani.

Baada ya kusomewa shaka lake na kutakiwa kujibu kama ni kweli au si kweli, alikiri na kuongezea maelezo yafuatayo:
1. Yupo tayari kufa kwa ajili ya kuupigania uhuru

2. Ukoloni haujaisha nchini kwake Kenya

3. Wanatawaliwa na vichaa, waongo, na wezi

4. Alihoji kama jukumu la Serikali ni kulinda au kuua raia

5. Hawawezi kuendelea kuishi katika hofu

6. Kwa kipindi cha miaka 60 wameishi kama nusu binadamu

7. Wanatawaliwa na wachache
wasiojali maslahi ya wengi

Kwa ufupi, ni kama vile ameendeleza mgomo mpaka mahakamani!

Gen Z wenzake wa mataifa mengine ya Afrika watamwelewa?

 
Aendelee tu na msimamo wake sisi huku ni manyumbu hatutaki kufa,huku ni mwendo wa mitano tena na chama pendwa oyee hii Iko kwenye DNA zetu
 
Anajua anachokipigania, nampongeza. Yote anayosema ndiyo kila siku tunayapigia kelele. Karibu viongozi wote wa Afrika wanafanana. Kituo kifuatacho ni Uganda...
 
Kamau si generation Z,huyu mwamba ni Pastor na activists. Kwanza namuona kama anazidi kuwa kijana, mwamba kawekwa sana ndani, mwaka 2022 aliwasha moto kama kaawaida yake kabla ya mwezi uliopita kupinga treasurly cabinet.

Hawa ndio early people kwenye rise ya activism nyingi kenya na hapo yeye alikua anaongelea haki zaidi na sio madai ya generation Z ya sasa. Huyu anaongelea uhuru wa kuongea na kufanya mambo kenya.
 
Back
Top Bottom