Wito wa kuirudisha fainali ya Ngao ya Jamii 2023 mjini Dar es Salaam

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Ni jambo jema kupeleka mechi kubwa katika maeneo tofauti ili watu wa maeneo ya huko ambao huwa hawana nafasi ya kuziona mechi kama hizo waweze kupata fursa hiyo. Shida kubwa inakuja kuwa viwanja hivyo haviandaliwi vizuri ili viendane na hadhi ya mechi husika. Ingekuwa vyema mechi kama hizi ambazo nyingi huwa zinajulikana mapema, ziende na uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya maeneo husika ili ladha ya mechi isipotee na wenyeji tuwaache na kitu watakachokitumia baada ya mechi husika kuisha.

Tukumbuke sababu tuliyopewa ya kupeleka mechi zote za ngao ya Jamii Tanga ni kwamba uwanja wa Benjamin Mkapa uko katika matengenezo. Tunajua sehemu ya pitch kwa kiasi kikubwa matengenezo yake yatakuwa tayari yameisha au yako mwishoni maana tuliona mabadiliko makubwa katika pitch wakati wa mechi za mwisho mwisho za Yanga za shirikisho na zile za timu ya taifa dhidi ya Uganda na ile ya Niger. Cha kushangaza tofauti na taarifa tulizopewa na TFF, tumeambiwa siku ya sherehe za Yanga wiki ijayo zitafanyikia uwanja huo huo ikiwemo mechi kati ya Yanga dhidi ya Kaizer Chiefs. Hii inaashiria maboresho yanayoendelea pale hayazuii shughuli zingine kuendelea ikiwemo mechi kubwa kuchezwa.

Mechi zote 3 za mwaka huu za Ngao ya Jamii ni mechi kubwa na zitakazovutia watu wengi kuzifuatilia. Nashauri ili kulinda ladha ya mechi husika na pia kutoa fursa za watu wengi zaidi kuhudhuria, mechi hizo titawanywe katika miji tofauti. Tanga wabaki na mechi moja (kama ikibidi), nyingine ipelekwe Mbeya au Morogoro maana ni muda maeneo haya hawajapelekewa mechi kubwa kama hizi na fainali irudishwe Dar es Salaam. Mechi ya mshindi wa tatu iondolewe.

Uwanja wa Mkwakwani hauwezi kuhimili kutumika kwa mechi 4 mfululizo ndani ya muda mfupi kama ratiba ilivyotolewa inavyosema. Ikifika fainali ile pitch itakuwa kwenye hali mbaya sana na tutashuhudia fainali mbovu na pia uwezekano wa wachezaji kupata majeraha kwa sababu ya ubovu wa kiwanja.

Pia natoa rai kwa TFF kama taasisi ya umma waache tabia ya kudanganya na kutoa taarifa za uongo ili tu maamuzi yao yaweze kukubalika ambayo mengine yanaonekana yanafanywa kwa maslahi binafsi ya watu fulani.

FAINALI YA NGAO YA JAMII 2023 IRUDISHWE DAR ES SALAAM.
 
Tukisema ubovu wa Karia watu wanamtetea. Lakini huyu ni jipu.
 
hizi timu viongozi wake Wana funza kichwa I, wanakubalije upuuzi kama huu
Kupeleka mechi nne kubwa katika uwanja mmoja ambae tena hauna miundombinu ya kutosha ndani na nje ya uwanja kuweza kumudu ni dhahiri kulikuwa na uwalakini katika maamuzi hayo. Kuna shida mahali ila nadhani kutokana na Yanga kutangaza kufanyia shughuli yao taifa, muda bado upo kulirekebisha hili jambo.

Tuendelee kupaza sauti.
 
Acheni chuki bora karia anapeleka mechi ila yule malinzi alijenga uwanja wa kisasa kila mtu alikaa kimya.
 
Kujenga uwanja hayo ndiyo maendeleo ya maana yaliyo kwenye hoja hii siyo kutafuta sifa huku ukienda kuharibu burudani inayosubiriwa. Kama anataka mechi za kutosha ziende huko Tanga ajenge uwanja wa kisasa wenye pitch nzuri na unaochukua idadi ya kutosha ya watazamaji. Akifanya hivyo, timu zenyewe tu zitataka kwenda kucheza kule, na wengine kufanya pre-season na hadi wawekezaji wa mahoteli wataongezeka na kutatua shida nyingine ya malazi iliyopo kule inayoonekanaga shughuli ya watu wengi inapopelekwa Tanga.

Mechi ya mshindi wa tatu inafanyika masaa 2 kabla ya mechi ya fainali kwenye uwanja huo huo, umeona wapi hili jambo kufanyika kwa timu kubwa za hadhi ya timu hizi? Si mambo ya UMITASHUMTA haya?
 
Kupeleka mechi nne kubwa katika uwanja mmoja ambae tena hauna miundombinu ya kutosha ndani na nje ya uwanja kuweza kumudu ni dhahiri kulikuwa na uwalakini katika maamuzi hayo. Kuna shida mahali ila nadhani kutokana na Yanga kutangaza kufanyia shughuli yao taifa, muda bado upo kulirekebisha hili jambo.

Tuendelee kupaza sauti.
Mi nakuunga mkono, huu ni zaidi ya uhuni.
 
Nililisema hili la uwanja watu wakaona jambo siyo kubwa kihivyoo, sasa malalamiko kila mahali kuhusu uwanja. Sasa wasubiri Jumapili mpira utakavyokuwa mbovu. Atapigwa mtu goli 4, malalamiko yote yatakuwa kuhusu uwanja.
 
Tena itaanza kuchezwa game ya mshindi wa Tatu, then ndo final ifatie the same day, asee hali ya uwanja sijui itakuwaje yani..
 
Back
Top Bottom