Wito wa kukomeshwa viboko mashuleni, Tanzania

Wito wa kukomeshwa viboko mashuleni, Tanzania

Dunia inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko shuleni leo. Nchini Tanzania, baadhi ya mashirika ya haki za binadamu na yale yanayojihusisha na elimu yametoa tamko la pamoja yakisisitiza umuhimu wa kuondoa adhabu hiyo katika mazingira ya shule.

Tamko hilo pia linaungwa mkono na mashirika ya kimataifa yanayoshughulika na ustawi wa watoto, yakiwemo lile la Watoto, UNICEF na Shirika la Afya Duniani, WHO.
View attachment 3582099

Source: DW Kiswahili
Kwani Adhabu ya viboko mashuleni, makosa yake ni yapi?
 
Hii sheria ya kuruhusu viboko ikiondolewa, balaa lake litakua ni kubwa sana kwenye kipengele cha nidhamu na ufaulu kwa shule nyingi za Kata kote nchini.
 
Hii sheria ya kuruhusu viboko ikiondolewa, balaa lake litakua ni kubwa sana kwenye kipengele cha nidhamu na ufaulu kwa shule nyingi za Kata kote nchini.
Ingewekana viboko vilitakiwa viwe mpaka vyuoni maana watoto wanatoka sekondari wakiwa na nidhamu ila wanaenda kuharibikia vyuoni kwa sababu ya kupewa uhuru na kutopigwa.
 
Viboko chuoni? Mawazo ya kijinga
Na sio chuoni tu mpaka kwenye ofisi za wizara na ikulu viboko vilitakiwa viwepo maana huko ndo kumejaa wapumbavu na watia hasara taifa kuliko hata huko shuleni.
 
Inawezekana endapo watalipa ada. Hiyo itasaidia wazazi kuwa responsible
 
Back
Top Bottom