Wito wa Waziri wa Fedha Mwigulu, juu ya Wazazi kuwasaidia watoto wao kujiajiri uko sawa!

Wito wa Waziri wa Fedha Mwigulu, juu ya Wazazi kuwasaidia watoto wao kujiajiri uko sawa!

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2016
Posts
2,097
Reaction score
1,457
Wito wa Waziri wa Fedha, juu ya Wazazi kuwasaidia watoto wao kujiajiri uko sawa! Anaebisha aseme!
Yupo Sahihi kabisaa maana ukiangalia hawa wazazi ni mfano wa kuigwa kwake....

1. Samia amemsaidia mtoto wake kujiajiri kwani binti yake mmoja ni Mbunge na mkwe wake ni Mbunge na ni Waziri (Mchengerwa) na mwingine juzi ameukwaa uongozi wa ndani ya ccm.

2. Mzee Mwinyi Kamsaidia mtoto wake kujiajiri maana mmoja wa watoto wake ni Rais wa Zanzibar.

3. Mzee Kikwete Kamsaidia mtoto wake kujiajiri kwani ni Mbunge na ni Naibu waziri ardhi na mke wake ni Mbunge...

4. Mzee Makamba Kamsaidia mtoto wake kujiajiri maana ni Mbunge na ni Waziri wa wizara ya giza...
5. Mizengo Pinda kijana wake amemsaidia kujiajiri ni Mbunge na ni naibu waziri wa katiba na SHERIA.
6. Edward Lowasa amemsaidia kijana wake pia kujiajiri ni Mbunge wa Jimbo huru la Monduli
Unataka mifano gani mingine na mingapi ndo uelewe hoja ya huyu jamaa??

Sasa wewe mzazi kwa kimpungua, mgori, mampata nk kaa hapo usubiri hawa jamaa wakutengenezee ajira za watoto wako kama hujasaga meno...
 
Jamaa limechoma kwenye mshono..

We somesha mtoto wako ila kama unasubiri Sisiemu imtengenezee ajira niite wuh wuh 🐶🐕🐶🐕 niko pale nime🐕‍🦺
Alafu ukikutana na vibabu vya Chichiem vinakuuliza Shule uliyosoma kajenga babaako, unauliza nini wewe, " Vizee vya Chichiem ni vichungu""
 
Madelu chenga sana, keshavimbewa na asali anabwabwaja lolote lile....
 
Hapa wazazi wamedhihakiwa na Mwigulu kwa mara nyingine, yeye hajawahi kujiajiri mpaka alipowekwa hapo wizara ya fedha
 
Wito wa Waziri wa Fedha, juu ya Wazazi kuwasaidia watoto wao kujiajiri uko sawa! Anaebisha aseme!
Yupo Sahihi kabisaa maana ukiangalia hawa wazazi ni mfano wa kuigwa kwake.

1. Samia amemsaidia mtoto wake kujiajiri kwani binti yake mmoja ni Mbunge na mkwe wake ni Mbunge na ni Waziri (Mchengerwa) na mwingine juzi ameukwaa uongozi wa ndani ya CCM.

2. Mzee Mwinyi Kamsaidia mtoto wake kujiajiri maana mmoja wa watoto wake ni Rais wa Zanzibar.

3. Mzee Kikwete Kamsaidia mtoto wake kujiajiri kwani ni Mbunge na ni Naibu waziri ardhi na mke wake ni Mbunge...

4. Mzee Makamba Kamsaidia mtoto wake kujiajiri maana ni Mbunge na ni Waziri wa wizara ya giza...
5. Mizengo Pinda kijana wake amemsaidia kujiajiri ni Mbunge na ni naibu waziri wa katiba na SHERIA.
6. Edward Lowasa amemsaidia kijana wake pia kujiajiri ni Mbunge wa Jimbo huru la Monduli
Unataka mifano gani mingine na mingapi ndo uelewe hoja ya huyu jamaa??

Sasa wewe mzazi kwa kimpungua, mgori, mampata nk kaa hapo usubiri hawa jamaa wakutengenezee ajira za watoto wako kama hujasaga meno...
Mwigulu Nchemba hebu tuambie ni lini ulipojiajiri? Hata hayo mabasi umeyapata ukiwa ni mwajiriwa
 
Siyo suala la kukumbushwa ila ni msemo wa dunia hii

"Hakuna utajiri kwenye kuajiriwa labda fisadi kama mwigulu na wenzake"

"Kama mnaitaka mali mtaipata shambani (kujiajiri)" ndiyo neno lenye afya
 
Nyongeza magufur alimtimua hivi sasa anafidi makovu akija kutoka deni la taifa 150 trillions
 
Hii ni call kwa vijana wa Tanganyika ya kuamka na kuukataa usingizi unaoitwa amani! Ni Bora call hiyo ingeitwa ajira kidogo ingesound better!

Humu ndani Kuna vijana njaa Kali wasiopisha kitu kinaitwa pesa kwani hata jero kwao ni Bora kuliko uzalendo!

Wapo tayari kuwashambulia wenye mtazamo Bora wenye kuibeba kesho yao kwa malipo kiduchu! Hawa mnawaita chawa ni tishio la kutofikia ndoto zenu kwani ni wabemendaji wa mawazo chanya yenye uelekeo Bora wa kesho yenu.

Amkeni na mkaikatae CCM ya undugunaizesheni na mkalete mabadiliko ya kweli kwani sisi wengine tulivuka huo uzee tupo kwenye ukongwe na huenda kuiona 2025 ikawa bahati ya mtende!
 
Watawal a wa sheria Wana andaa watoto wao kuwatawala watawaliwa wa sheria.
KILA kinachoendelea jua si bahati mbaya ni mipango kabisaa.
Silaha Yao kubwa ni shule zinazouwa uwezo binafsi wa watoto kutafakari na kuwafanya kuwa tegemezi wa mawazo ya jumla na kutojiamin... Hii ikikomaa tarajia walemavu kama HALI ilivyo sasa na kuendelea.
#Hakikisha mwanao ni mtu wa kuhoji KILA anacholetewa usoni
 
Acha kuwapa credit na sifa kizembe hawana akili hio ya kuharibu mfumo mzima wa elimu kwa faida zao binafsi[emoji23]
 
Back
Top Bottom