Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
Na Victor Kinambile, Tabora
KATIKA hali ya isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana aliwaambia wananchi kuwa wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja na vikongwe nao hawana budi kuuawa kwa kuwa wakisubiri mahakama kuwahukumu, watakuwa wanakosea.
"Mkimuona mtu akamkata mwingine shingo naye muueni kwani sasa viongozi wote tumechoka... no more, I can't tolerate anymore (imetosha, siwezi kuvumilia tena)," alisema Pinda huku akiwaacha watu midomo wazi.
Pinda anatumia chama chake:-
"Umoja wa vijana wa CCM mna jeshi zuri ambalo naamini mkiamua mnaweza kutokomeza mauaji ya wazee wetu pmoja na ndugu zetu maalbno na kazi hiyo nawaagiza muanze leo msisubri auawe mwingine tena," alisema waziri mkuu.
Waziri Pinda alisema iwapo wananchi wataendelea kuwahurumia wauaji hao ambao wanatafuta viungo vya albino wakitegemea mahakama itatenda haki huku nao wakiongeza kasi ya mauaji kwa Watanzania, watakuwa wanakosea.
Hivyo alisema kwamba kuanzia sasa mtu yeyote atakayemuona mtu amemkata shingo au mkono mweziwe basi naye auawe papo hapo hii itakuwa ndiyo dawa kwani vingozi wote tumechoka na mauji hayo.
---------------------------
Hivi hapa ni kiongozi wa Chama au wa Serikali na ndivyo Kama Waziri Mkuu alitakiwa kutoa kauli hii ? Je Waziri wa Ulinzi yupo wapi ? Kama mauaji yanaendelea inamaana mkuu wa Jeshi la Polisi,Mkuu wa Upelelezi na Waziri wao hawafai ,hivyo ilibidi wawajibike au yeye Waziri Mkuu awawajibishe na sio kutoa kauli za vitisho na kuwafanya wauaji wawe makini zaidi wanapotekeleza mauaji yao. Na pale aliposema ....Viongozi wote tumechoka..... WaTanzania mnaichukuliaje kauli hii ya Kiongozi Mkuu wa Nchi kutangaza kuwa yeye na wenzake wamechoka.

Last edited by a moderator: