Kwa siku kadhaa sasa hivi kile ambacho alisema Waziri Mkuu kuhusu wauaji wa Albino kinabakia kuwa siri kubwa. Kumekuwa na jitihada za makusudi kabisa kuficha alichosema Waziri Mkuu.
Jana katika taarifa ya habari ya saa mbili (za usiku) TBC ilizungumzia jinsi NCCR ilivyotoa tamko la kulaani mauaji ya Albino. Wao wakaongezea na kusema kuwa Waziri Mkuu alisema kuwa wale wanaohusika na mauaji ya Albino "washughulikiwe kwa mujibu wa sheria".
Nimepata nafasi ya kuzungumza na watu wengi weekend hii kupata hasa alichosema Waziri Mkuu karibu wote wanazungumzia kile "alichomaanisha". Nimegundua hakuna anayesema hasa kile "alichosema".
Je ni kweli Waziri Mkuu alitoa kauli hizi kama zilivyonukuliwa na Mwananchi?:
a. Mkimuona mtu akamkata mwingine shingo naye muueni kwani sasa viongozi wote tumechoka... no more, I can`t tolerate anymore (imetosha, siwezi kuvumilia tena
na hii hapa kuhusu UVCCM kushiriki katika kukomesha mauaji ya albino, labda kwa kuangalia (a) hapo juu.
b. Umoja wa vijana mna jeshi zuri ambalo naamini mkiamua mnaweza kutokomeza mauaji ya wazee wetu pmoja na ndugu zetu maalbino na kazi hiyo nawaagiza muanze leo msisubri auawe mwingine tena
Naamini hakuna "maelezo" au "taarifa kwa vyombo vya habari" ambayo inajibu swali la nini hasa Waziri Mkuu alisema.
Kuna njia moja tu ya kuamua kwa haki kauli ya Waziri Mkuu ilikuwa ni ipi hasa maana uwezekano kuwa Waziri Mkuu wetu akizungumza kwa niaba ya "viongozi wote" na kwa jina la serikali kwamba amewaambia watu wa kijijini kuwa wanaweza kuua with impunity inatisha. Hofu yangu siyo kwa wasomi wa kisheria na watu ambao wanaweza kuelewa "alichomaanisha" bali wale watu ambao walikuwa wanamsikiliza walisikia nini hasa.
Sisi wengine wanaweza kutuzuga kuwa alimaanisha nini lakini wale Sungusungu, na wanakijiji kule Shinyanga walivyomsikia watakuwa na utata wowote wa kuelewa alichomaanisha?