Huu ulikuwa ni mkutano wa hadhara, wewe muandishi wa habari huwezi kusema alichosema Waziri Mkuu kinafichwa! Kituko!
Huwezi kutegemea, huwezi kusubiri, Ofisi ya Waziri Mkuu ikupe nakala ya hotuba, offcourse wataifanyia ukarabati!
Ni sawa na kusema waandishi na wabunge wanasubiri Ikulu itoe nakala ya hotuba ya Rais. Kwani hiyo hotuba alipoitoa alikuwa amejifungia chumbani na familia yake???? I mean, how preposterous is that?
Mkutano kuhusu the most pressing issue at the time, mauaji ya albino halafu hakuna press person hata mmoja aliyekuwepo, au aliyekuwa na ki-recorder. Makampuni ya uandishi Bongo yanashindwa kuwa na ki-SONY recorder cha dola 40 cha Best Buy?
Crummy crummy crummy press!
Hata Mwakyembe jana ame vindicate ninacho ki-guess kila siku humu kwamba waandishi ni watoto wa shule. Mwakyembe kasema mwandishi wa MwanaHALISI aliyemnukuu juzi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Nyegezi. Exactly what I was fearing. I mean, I knew these could not be seasoned press people. Absolutely impossible. Journalism in Tanzania is the shoddiest profession of all.
Hakuna anaejua Pinda katamka nini Mwanza. Hakuna anaejua Mkapa katamka nini Zanzibar with this "kakiri makosa" story. Hakuna anaejua Mwakyembe katamka nini Mbeya juzi akiwacharura wapinzani. Matokeo yake ndio inabidi ukamuulize Mwakyembe mwenyewe "eti ilisema hukusema"? Offcourse atakuyeyusha, atakupa tafsiri mpya kama anavyojisikia, utamuitikia itikia hapo wee, halafu anakuona hujui lolote anakupa sasa mpaka tafsiri za Pinda wakati yeye mwenyewe hakuwepo, na wewe na mimi msikilizaji wote hatukuwepo, na yeye unaemuuliza anasema hajui kilichosemwa. But he is good enough kukutafsiria. Labda sasa tuwaombe kina Shekhe Yahaya wawe wanatuambia yanayosemwa popote pale kwa kutumia some telepathic means or something. Nobodies knows nothing. Press yetu masikini weee!
"Kuna jitihada za kuficha alichosema Waziri Mkuu..."!
Such cheesy press!
Sikubaliani na wewe kabisa kwa hoja hii "Journalism in Tanzania is the shoddiest profession of all." Ila ninachojua you are arguing from ignorance of what journalism is and what it entails! Kama unayosema kuhusu waandishi wa habari ni kweli basi viongozi wetu wengi (au tu Watz wengi) wangekuwa kwenye taaluma ya uandishi wa habari kwa kuona namna wanavyowajibika au ripoti kuhusu matukio fulani fulani kwenye sehemu zao za kazi!
Mwandishi wa habari anaweza kuripoti ukweli fulani lakini ukakanushwa kwa makusudi na kwa bahati mbaya ukikanushwa kwa namna hiyo, huyo mwandishi wa habari ataonekana mwongo. Lakini anayekana ukweli ataonekana yuko sahihi.
Mwandishi wa habari anaweza akakatazwa kuripoti tukio fulani kwa vile linagusa maslahi ya watu fulanifulani au hata kama ataripoti owner wa gazeti anamwambia editor wake kuwa stori fulani isitoke kwenye gazeti lake au kama ikitoka anapewa nakala tofauti na ile ya mwandishi wa habari. Haya yanafanyika! Baadhi ya viongozi wana waandishi wao na hawataki mwandishi mwingine yeyote na kabla ya kuripoti kitu wanaambiwa kitu gani waandike.
Na ujue mwandishi wa habari anapoleta stori kwa editor siyo yeye (mwandishi wa habari) tena anayeamua hiyo stori itoke hivyo au ibadilishwe. Je, wewe ungekuwa mwandishi wa habari katika mazingira hayo ungefanya nini - yaani ulichoandika hakitoki vile na kama kikitoka unakuta kimebadilishwa baadhi ya 'contents' zake?
Hivi unakumbuka alivyosema ex-Waziri Mapuri wakati waandishi wa habari walipopigwa na askari magereza hapa Dar miaka michache iliyopita? Mambo yalipopamba moto Mapuri alikanusha na kusema alikaririwa vibaya na vyombo vya habari - namna tu ya 'defence mechanism'.
Unakumbuka pia wakati ugongwa wa Mafua ya Ndege au Rift Valley (sikumbuki vizuri ulikuwa ugonjwa gani nimesahau) ulivyotesa muda fulani Dodoma na vyombo vya habari viliripoti, lakini baadaye waziri fulani alikanusha na kusema ni uongo? Ila mambo yalipoendelea kuharibika waziri huyohuyo alitangaza ugonjwa huo kuwa 'janga la kitaifa'.
Unakumbuka pia kulitangazwa kuna njaa Singida au Arusha (sikumbuki vizuri pia ni mkoa gani kati ya hiyo 2) miaka michache iliyopita na kwamba mtoto mmoja alifuka kwa kukosa chakula lakini waziri fulani akakanusha na kusema alikufa kwa 'malnutrition' na siyo njaa? Yaani yeye alijidai anajua kilichomwua mtoto kuliko hata mama mzazi aliyekuwa hana chakula nyumbani.
Siku moja nilipita kituo fulani cha polisi hapa Dar na kukuta askari wa kike amemkaba bwana mmoja shingoni akimtolea lugha chafu na kusema 'leo utanikoma'. Kwa vile dirisha lilikuwa la vioo na nilikuwa karibu niliona kilichokuwa kinafanyika.
Huyo bwana alikuwa akiomba radhi lakini huyo askari wa kike alisema tu 'leo nimekwambia utanikoma'! Askari wadogo walijitahidi kusuluhisha lakini aliwakemea akiwaambia wao ni askari wadogo tu hawawezi kumwambia kitu. Hivyo aliendelea kumwonyesha huyo bwana uwezo aliokuwa nao juu yake.
Na watu wengine pia walikuwepo na nilienda pale kituoni kuuliza kama kuna kitu kama hicho. Askari wa zamu alinijibu kila kitu kilikuwa swari na hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa amekabwa vibaya na askari. Pia alisema kama nikitaka maelezo zaidi niende kuuliza Central Police Station kwa vile pale kituoni hawakuona kitu chochote. Hivyo nilishindwa kupata habari yoyote ya huyo (bwana harusi mtarajiwa aliyekuwa ameenda kwenye kikao cha harusi karibu na kituo cha polisi na kuangukia pabaya).
Uandishi wa habari ni taaluma sawa na taaluma zingine lakini ni taaluma taofauti pia. Mtu anaweza kuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza na akawa mwandishi wa habari na mwingine akawa profesa mwenye zaidi ya PhD 10 na asiwe mwandishi wa habari.
"... But one thing is common to the job of all journalists: they are all communicators. They are gatherers and disseminators of information, eager to share their knowledge and insight with members of the public thirsting for understanding... [a journalist] is an explorer, venturing where we sometimes fear to go - places of danger and splendor... When necessary journalists act as shapers of opinion - as the moral conscience of the nation - expressing general public outrage over injustice, cruelty or stupidity by those in power... " (Journalism Notes - The Writers Bureau College of Journalism, Manchester - UK).
Jounalists ni watu wanaojituma sana na wanafanyakazi kwenye mazingira magumu mno. Lakini sisi Watz tumejazwa tu na 'prejudice' kuhusu hawa watu na kwa bahati mbaya wakiripoti kitu ambacho ni sahihi na baadaye kikikanushwa na wakubwa kwa sababu fulanifulani za kisiaza tunaona wao ndio hawajui - hawana elimu!
Kwani kusema PM Pinda kasema hivi au vile kuhusu albinos unahitaji uwe na digrii ngapi au uwe mwaka wa ngapi chuoni? Mbona sources wenyewe wa habari wanaweza hata wakawa watoto wa chekechea, shule ya msingi nk?
However, kunaweza kuwa na 'factual errors' katika reporting, pengine kwa sababu watu waliotakiwa kuthibitisha walificha baadhi ya information. If that happens haina maana kwamba basi hii taaluma ni bure kabisa - 'shoddist of all professions'.