Wito wangu kwa waalimu wapya wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Ndala ndefu

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2012
Posts
237
Reaction score
42
Ndg waalimu naimani mu-wazma wa afya! Habari za uhakika nilizonazo ni kuwa kwa waalimu wote tulioajiriwa mwezi march mwaka huu wilayani Magu waalimu watakaopata mishahara ya mwezi huu hawazidi 20, wengine tutaendelea kushughulikiwa taratibu! Wito wangu kwenu ni kuwa siku ya j,nne tukutane pale Bomani tuonane na Mkurugenzi elimu na tukatae kurudi ktk vituo vyetu vya kazi bila kulipwa. Kumbuka tulipewa pesa ya kujikimu kwa siku 7, je tutawezaje kuishi maisha ya ugenini bila fedha? Tumepanga vyumba, tunahitaji nauli za kwendea makazini na kurudi nyumbani kwetu pia huwezi kuingia darasani kufundisha bila kula. Nawaomba waalimu tuungane ktk hili, sio wilaya ya Magu pekee bali watanzania wote tunaomba mtuunge mkono! Asanteni
 
Mhh... Ile mizengwe ya miaka nenda rudi kumbe haijakoma. Mungu saidia mpambane kwa hoja, si kwa nguvu.
 
Wameanza ubabaishaji wao na hali pesa ya kujikimu wamechakachua, itakula kwao ktk matokeo na wataishia kuunda tume daily.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…