Ndala ndefu
JF-Expert Member
- Dec 24, 2012
- 237
- 42
Ndg waalimu naimani mu-wazma wa afya! Habari za uhakika nilizonazo ni kuwa kwa waalimu wote tulioajiriwa mwezi march mwaka huu wilayani Magu waalimu watakaopata mishahara ya mwezi huu hawazidi 20, wengine tutaendelea kushughulikiwa taratibu! Wito wangu kwenu ni kuwa siku ya j,nne tukutane pale Bomani tuonane na Mkurugenzi elimu na tukatae kurudi ktk vituo vyetu vya kazi bila kulipwa. Kumbuka tulipewa pesa ya kujikimu kwa siku 7, je tutawezaje kuishi maisha ya ugenini bila fedha? Tumepanga vyumba, tunahitaji nauli za kwendea makazini na kurudi nyumbani kwetu pia huwezi kuingia darasani kufundisha bila kula. Nawaomba waalimu tuungane ktk hili, sio wilaya ya Magu pekee bali watanzania wote tunaomba mtuunge mkono! Asanteni