Katika pita pita yangu mitandaoni, nimeona ndugu zetu, majirani zetu, watani zetu wa Kenya wana uhaba mkubwa wa chakula hasa nafaka.
Nashauri, kwa kuwa sisi tuna chakula kingi na kwa kuwa kuna ugumu sana wa kupitisha mizigo kwenda Kenya na wao kufuata huku sababu ya janga la korona.
Serikali iweke utaratibu wa wafanyabiashara wetu kuwafikishia mzigo mipakani na wao wanunue hapo.
Hiyo ni kwa sababu Nairobi na Kenya kwa ujumla ina upungufu mkubwa wa nafaka inayopelekea wananchi kuhatarisha maisha yao kuvuka Tanzania kuchukua chakula.
Naomba watanzania wenzangu tuwasaidie hawa jirani zetu ambao ni watani zetu wa jadi maana huwa tunabishana kuhusu kila kitu ila bado tunapendana.
NB. Wale mliopungukiwa chakula majirani naweza kuwasaidia magunia kadhaa ila sijui mzigo utawafikiaje huko...