WIVU: Maana, faida na hasara zake

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
3,811
Reaction score
1,607
Wakuu Wana JF, Salaam!
Nimejaribu kuangalia kama hii mada ilishaletwa hapa lakini sikuona inayolingana nayo. Ikiwa ipo tayari samahani kwa kuirudia.

Huwa ninatatanishwa na dhana ya WIVU katika mapenzi. Naomba mjadala:
1. Nini maana ya wivu?
2. Kwa nini (baadhi ya) binadamu wanakuwa na wivu kwa wapenzi wao?
3. Wivu ni kichochocheo au kiuwaji cha mapenzi?
4. Ni kiwango/aina gani ya wivu kinakubalika katika mapenzi?
5. M'mke/M'mme asiye na wivu huwa hampendi mpenzi wake?

Ingawa nimeweka nambari lengo ni kufafanua wasiwasi wangu, hakuna ulazima wa kuchangia kila hoja katika nambari.

Jumapili Njema kwa wote.
 
Wivu ni kitu cha asili kilichowekwa na Mungu tangu mwanzo, Kumbuka Mungu alipowafukuza Adam na Eva katika bustani ya Eden, Mungu alimwambia Eva tamaa yake itakuwa juu ya Mumewe, Kwa hiyo hiki kitu kipo naturaly

Na kama mtu hana wivu kwa mkewe/mumewe ujue kuna walakini fulani.
 
Wivu ni kichocheo cha mapenzi japo kikizidi huwa ni kero kwa muhusika
 
ni kweli wivu ni njia moja wapo ya mapenzi ya dhati kwasababu bila kuwa na wi kwa mpz wako utakuwa ujampenda.mfano unaweza ukakuta sms za mapenzi kwenye cm ya mpz wako lazma utapanic na utauliza kitendo cha kuuliza ni moja wapo ya wivu.
 
Jamani,sina amani na simu yangu,mwanaume asinipigie,naulizwa kwanini ananipigia?anataka nini?napigwa,natukanwa kisa kupigiwa na mwanaume.jaman nifanyeje?mana katika wanawake wakwel,nimekuwa mkwel sana sijawah kucheat lakin nitaambiwa natafuta wanaume.namwelewesha lakin haelewi.jaman kama ni wivu,wivu gan huu?nimwache?naumia mana nawaza kupitiliza,na tatizo la huyu mwanaume.nisaidieni mawazo wanajf
 
sasa dada angu yaani unatukanwa,unapigwa afu unakuja JF kuomba ushauri.................kusoma hujui hata picha tu?
 
Hao wanaume wanakupigia nini wakati ukiwa na mumeo... Hata mi ningemaindi aisee, by the way huwa namaind na nilishawahi kumchapa mtu mabao na kuvunjavunja simu na line yake...
 
wanakupigia wakati gani?kwa mazungumzo gani? kama ya kikazi nitamshangaa pia, lakini kama simu inapigwa wewe unajiumauma kuongea, au inapigwa usiku bila kuwa na mazungumzo ya maana, mara ooh nilikuwa nakusalimia tuu....aaahh jamani...........muache baba wa watu akutandike tuu
 
pole, wacha aendelee kukupiga mpaka akung'oe macho, mapenzi gani ya kubondana
 
Hapo unataka ushauri gani? Labda hiyo ndio aina ya mapenzi mliyoichagua, nawatakia kila la kheri.
 
kabla sijakushauri naomba unisaidie yafuatayo
1)mida unayopigiwaga hizo simu
2)huwa unazipokelea mbele yake/unajificha??
 
We yaelekea ni kicheche,wacha ubondwe 2.
 
Uchungu wa mke ajuaye mume,usimsababishie hayo machungu
 
tupa simu...!!
 
Hao wanaume ni kina nani na mnaongea nini? Kukupiga siungi mkono; lakini kama unapokea simu za wanaume now and then hata mimi sioni kosa la mumeo kukuhoji. Mambo ya kazi yaishie kazini ukiwa na mumeo mnahitaji quality time. Respect his feelings.
 
kabla sijakushauri naomba unisaidie yafuatayo
1)mida unayopigiwaga hizo simu
2)huwa unazipokelea mbele yake/unajificha??
Kwa kuongezea maswali:
3) wanaokupigia ni wanaume wa aina gani?
4) Jee yeye hapigiwi simu na wanawake? Kama anapigiwa, ni wanawake wa aina gani?
Ikiwa nyote mnapigiwa na jinsia zilizo nje ya familia zenu, inaonesha nyote wawili hamjatulia.
PLAN A: Mkalishe mlizungumze hilo na kuwekeana masharti ya nani na nyakati za kupigiwa simu.
PLAN B: Tit for tat. (Pengine mume wako ni mkorofi na plan A haitaki), akipigiwa simu na mwanamke mpe kisago kimoja cha nguvu (frying pan juu ya kichwa ni silaha nzuri) angalau aonje uchungu wa maumivu unayoyapata.
 
punguza mawasiliano yasiyokuwa na umuhimu.. kuna watu wa ajabu sana! anampigia simu mke/mume wa mtu zaidi ya saa2:30 usiku kwa ishu ambayo ingeweza kusubiri kesho

au anapiga simu hana jambo la maana zaidi ya kuongelea mambo yasiyokuwa na msingi sasa mme/mke akisikia maongezi yale tena mara kwa mara anaanza kuhisia hisia. Lakini ni wewe unaemplekea kukuhisi vibaya.. ndo maana wadada wengi wakishafunga ndoa tu wanatupa line, anaanza upya
 
Akipigiwa simu na mwanamke mpe kisago kimoja cha nguvu (frying pan juu ya kichwa ni silaha nzuri) angalau aonje uchungu wa maumivu unayoyapata.
Mzee ukiruhusiwa kumiliki bunduki mbona itakuwa kasheshe. Hapo kwenye red umeniacha hoi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…