Wivu wa Diamond ni zaidi ya "Mke mwenza"

Youngblood

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
19,433
Reaction score
56,810
Najua wenye team zenu mtapanik sana tu,

Ila kama aliyosema Ommy dimpz leo kweny kipindi cha XXL huko clouds FM ni kweli, basi huyu bwana mdogo wivu wake ni wa kiwango cha juu sana, na hizi tabia za kitoto ambazo anazifanya ili tu kusababisha wenzake waonekane hawana maana kwa kweli ni hujuma kubwa sana,kwanini anapenda kufanya wenzake waonekane wabaya katika jamii ikiwa yeye amefanikiwa zaidi yao?

Naomba mshaurini ajirekebishe mapema kwani mafanikio hayaletwi na fitna na kama riziki ipo basi ipo tu haiwezi kizibwa na ungo.
 
Kama madai ya ommy ni ya kweli!!!

Ila kama umemuelewa naomba nijibu hili,anasema alipanga kufanya collabo na davido daimind akamzunguka kurudi kwa iyanya akakuta tayari jamaa kafanya tena collabo!
Nini kilimzuia yeye kufanya collabo na hao watu ilhali mpaka leo davido na iyanya bado wanafanya mziki?
 
Unajua kama na wewe ulielewa vizuri ishu ni kwamba ommy alipanga kufanya collabo na hao wasanii lakini,ishu ikaja kutokea kwamba diamond amewakamata hao wasanii woye kwa wakati mmoja ilihali rafiki yake tayari alishapanga kufanya nao,lakini pia ishu ya diamond kupanda dau kutoka $3000 ya ommy hadi $5000 ili tu ampiku best yake kwenye kolabo ambayo ommy alishaiwahi haileti picha nzuri kwa best friends.
 
Kwa hiyo unajaribu kusema aliyo yasema Dimpozi ndio ukweli lakini aliyo yasema Diamond hasa kuhusu swala la michezo mibaya ni uongo? Kama aliyo yasema Dimpozi yanachukuliwa ni ukweli basi hata aliyo yasema Diamond ni ukweli..labda useme umetumia formular gani kubaini alicho sema Dimpoz ndio ukweli na alichosema Diamond ni uongo....

Hivi Dimpoz anayo yafanya hayakufanyi uonekane wewe huna tofauti na dada yako?
Hivi swala la mchezo mchafu Dimpozi ameliongelea? Na kama ameliongelea amesemaje?
Diamond alikuwa ni mtu wa kunyamaza sana laki ni sasa imetosha dawa ya moto ni moto.
Nampongeza sana sana Diamond kwa kuanza kuwapa haki yao wanao mchokoza dunia hii ukiwa mpole sana watu watakuchokoza sana na watakusumbua sana tena sana.

Ni mjinga pekee ambaye atashindwa kujua kuwa Dimpoz anatumika kumchokonoa Diamond na chakujiuliza kwanini Dimpoz ameanza haya sana baada ya kutoa wimbo na Kiba? Dimpoz anajua ni nani anayemtumikia lakini hatoweza kupambana na Diamond maana si size yake ni bora wanao mtuma waje wazi wazi kuliko kumtuma mtu dhaifu kama Dimpozi.
 
Kwani davido na iyanya wameacha kuimba?
 
Mtenda akitendwa huhisi kaonewa na akuanzae mmalize mlitaka diamond akae kimya kwani ye hana moyo shangilien punga lenu lakini linadaiwa milion kumi na mond mwambieni amlipe mond hapumulii mtu amlipe pesa yake.
 
Upunguani tu mtafkiri mnalipwa iyo mipasho kumbenayo ni burudani basi nilikuwa sijui mhaa kweli tunafikiri asilimia moja tu katika alizetu naanza kuamini wabongo wengi vichaa utafiti haukukosea
Yani watu dizaini zako sijui huwa mnawaza kwa kutumia nn jf ina majukwaa kibao umeacha yooote umekuja huku kwenye umbea afu huutaki umbea, pole sana
 
Yani watu dizaini zako sijui huwa mnawaza kwa kutumia ma wowowo jf ina majukwaa kibao umeacha yooote umekuja huku kwenye umbea afu huutaki umbea, pole sana
Haa haaa poleee! Nafkiri umejijibu vizuri mwenye akili timamu hawezi kumjadili mtu au watu akasema hiyo ni burudani
 
Yani watu dizaini zako sijui huwa mnawaza kwa kutumia ma wowowo jf ina majukwaa kibao umeacha yooote umekuja huku kwenye umbea afu huutaki umbea, pole sana
Angalia Diamond alivobebwa na davido,akapelekwa level zingne,ni kazi na davido ndiyo imemuweka mond pazuri,davido wa leo sio yule,domo mswahil wa uswahilini
 
Haa haaa poleee! Nafkiri umejijibu vizuri mwenye akili timamu hawezi kumjadili mtu au watu akasema hiyo ni burudani
Ni sawa na uende jukwaa la siasa afu hupendi wanavopost siasa sasa si uchawi huu
 

Yeye alifanya na j martins alisema..lakini ata ivyo was too late kuorganise tena collable instead alimwachia rikzi mwenzie maana alisema me najua akitoka yeye na mm ni njia moja tu..aliishia kuonekana kwenye vdeo ya bum bum..
 
Huyu atakuwa team Dimpoz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…