Wivu wetu uko kwenye kitu gani hasa?

Wivu wetu uko kwenye kitu gani hasa?

Ngekewa

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2008
Posts
7,705
Reaction score
1,288
Salaam zenu wanajamii. Miongoni mwa vitu vinavyotufanya tupendane ni mahaba, ukuruba (feeling to each other) maumbile (beauty), maingiliano ya kimwili (sex), matarajio (expectations) na mengine mengi.

Sasa wenzangu tunapoona wivu juu ya wenzetu wa karibu yaani mke/mume au boyriend/girlfriend huwa tunaona wivu wa kitu gani maalum kati ya vitu vinavyofanya tupendane?
 
Maisha ni kupigania na kupata mafanikio na mafanikio mengine zaidi. Wote tumeumbwa na uhitaji kwa kujitahidi tufanikiwe na kufanikiwa zaidi. Amazing enough tumeumbwa na feelinga za kutaka kuwa sawa kimaisha kwa watu ambao tunaona tuko kwenye level moja. Then again roho ya kustand out from the rest! Unapoona wewe hufanikiwi unahisi hapa pagumu, kisha anakuja mwenzio anapapita unaingiwa na inferiority complex na kuanza kuogopa macho ya watu. It would have been fine if huyo mwenzio asingepavuka, sasa wewe unaona ili iwe sawa kwako ni bora ufanye namna asipavuke.
Ndio maana kama una rafiki na yuko chini kimaisha unamsaidia kupigana ili muwe sawa...akianza kukupita mnagombana because deep down u always want them to be under you.
 
Shimo langu aingie mwingine
 
Mi ninaaambiwa simpendi eti kisa sina wivu naye, hebu niambieni jamani nifanyeje ili nionyeshe hata kawivu kidogo aanze kuamini nampenda kama kweli moyo unavyompenda
 
Wivu huja naturally....huwezi kuweka kidole chako ukasema kwa uhakika wivu ni kwa sababu ya mojawapo wa ulichotaja hapo juu. Ni mjumuisho wa kila kitu ndio unapelekea wivu.Hulka ya ku possess kile "kilicho chako" kwa ujumla wake wote.
 
Ni ubinafsi tu unaotusumbua. Hivi hamna jibu sahihi ujue..
 
hivi kuna cha kuonea wivu zaidi ya dushelele....au sijaelewa swali.....?

Sasa mbona tunapoomba dushelele na watu tunaojuwa kuwa wana watu wao tunakuwa na subira ya kungojea zamu zetu?
 
Wivu huja naturally....huwezi kuweka kidole chako ukasema kwa uhakika wivu ni kwa sababu ya mojawapo wa ulichotaja hapo juu. Ni mjumuisho wa kila kitu ndio unapelekea wivu.Hulka ya ku possess kile "kilicho chako" kwa ujumla wake wote.

Mzalendo, unachosema kinaingia akilini kwani tunakuwa hatuna wivu kufatia vitu vya wenzetu!
 
Sasa mbona tunapoomba dushelele na watu tunaojuwa kuwa wana watu wao tunakuwa na subira ya kungojea zamu zetu?

Kwa kuwa unajua kuwa yule ana mtu wake, akili na moyo wako umeviandaa tayari kukubaliana na hali. Kwa hiyo ni rahisi zaidi kushinda hisia za wivu.
Lakini uhusiano ukishaanza utataka awe wako peke yako na hisia za wivu zinastawi taratibu. Mwishowe huwa mnaanza vitimbi vya kumfanya mwanaume amwache yule mwenzako. Mara utamsingizia uongo kuwa anacheat.. mara kwa waganga kutafuta dawa ya kumdhibiti jamaa... nadhani mnaelewa.
 
Mi ninaaambiwa simpendi eti kisa sina wivu naye, hebu niambieni jamani nifanyeje ili nionyeshe hata kawivu kidogo aanze kuamini nampenda kama kweli moyo unavyompenda

Mpige marufuku kwenda kwa majirani, kwa kuanzia!
 
Back
Top Bottom