asante kwa mada yako nzuri inayofikirisha sana, mimi binafsi neno wivu huwa lina maana tofauti kabisa na jinsi ambavyo jamii hulichukuia kwamba ni kumpenda mpenzi wako kupitiliza, hapana, kwa mfano, ninapoona baahdi ya mienendo ya mpenzi wangu haiko katika misingi mizuri kama mahusiano ya kupitiliza na rafiki zangu na watu wengine suala ni kumrekebisha kwa manufaa yangu na yake pia kwa kumkanya ili kuepusha madhara, fedheha, na pengine aibu ambayo ingenipata baada ya yeye kugundulika kuwa na wapenzi ovyo ovyo na heshima kutoweka. so! kwangu wivu si kama nampendea sana no! bali namlinda na najilinda mwenyewe kwa mambo kibao hata magonjwa pia!!! ni hayo tu.