Wizara/Shirika/Taasisi gani ya serikali ina huduma bora kwa wateja mpaka unatamani taasisi zote zingekuwa kama wao?

Wizara/Shirika/Taasisi gani ya serikali ina huduma bora kwa wateja mpaka unatamani taasisi zote zingekuwa kama wao?

Polisi wanahudumia kwa haraka Sana.
Wafuasi na viongozi wa Chadema watakubaliana na wewe 100%. Sababu hata kama hawajafanya maandamano intelligentsia ya polisi inagundua madhara au faida yake na kuchukua hatua mara moja
 
Wakuu weekend inaendaje?

Huduma kwa wateja upande wa serikali imekuwa mwiba mchungu, kila kona malalamiko tu ya watoa huduma taasisi hizo kutoridhisha na matarajio ya wateja.

Tukiachana na malalamiko hayo, ni taasisi gani upande wa serikali inafanya vizuri upande wa huduma kwa wateja, yaani ukifikwa unasikilizwa fqsta na tatizo lako kupatiwa ufumbuzi, hakuna longo longo za sistim iz dauni wala nini, ukifika (ukipiga simu) watoa huduma wanakupokea kwa bashasha mpaka unaona nusu ya tatizo lako lishapata ufumbuzi, yaani unapewa huduma bora mpaka unatamani taasisi zote za serikali ingekuwa kama wao?!

Embu itaje hapa taasisi nyinginr zione haya na kuboresha huduma zao kuwa top notch👌✨️✨️
Mochuari
 
Zahanati Na Vituo vya Afya vinajitahidi pamoja Na changamoto zake
 
Nadhan Tanesco kwa sasa wana huduma nzuri sana, siku hisi hata transfoma likibutuka mna uhakika litatengenezwa
Miaka ya nyuma tulishawahi kukaa. Mwezi mzima tunasubiria transfoma litengenezwe
 
Taasisi ya Elimu.

Specifically, Walimu wa shule za Msingi na secondary. Ukiondoa matatizo ya kimfumo/Sera hawa raia wanajitahidi beyond limit kutekeleza majukumu yao.

Kuanzia kufundisha kwa wakati, Kufundisha overtime bila malipo, Kufuatilia wanafunzi kuliko wazazi wao, Kuna mahali walimu wanalipia mpaka ada baazi ya Wanafunzi.

Kwangu mm, Shule na walimu wao nawapa 8 out 10.
 
Back
Top Bottom