Muhula wa kwanza wa masomo kwa kidato cha tano unaanza Julai. Lakini baadhi ya shule binafsi zimekwisha kufanya udahili, kudai kishika uchumba kinachofikia hadi shilingi 1,000,000 ambacho hakirudishwi iwapo utaghairi kwenda kwenye shule hiyo. Shule hizo pia nyingine zimeshafungua muhula wao wa masomo, tofauti na utaratibu wa Serikali.
Tatizo lililopo ni kwamba, wazazi tunalazimika kulipa ada kushikilia nafasi kwa hofu ya watoto kupangiwa shule za Serikali zisizokuwa na sifa nzuri katika rekodi zao. Iwapo itatokea mwanao amepata shule ya Serikali yenye sifa, hela yako itakuwa imeliwa kama hutajiunga na shule hiyo ya binafsi. Kwa nini Serikali inakubali utaratibu huu ambapo wananchi wanatapeliwa fedha zao? Serikali pia inaambulia makapi ya wasio na uwezo wa kulipa na au waliochujwamakapi?