Wizara wekeni utaratibu mzuri kujiunga kidato cha tano

Jahom

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2008
Posts
351
Reaction score
32
Muhula wa kwanza wa masomo kwa kidato cha tano unaanza Julai. Lakini baadhi ya shule binafsi zimekwisha kufanya udahili, kudai kishika uchumba kinachofikia hadi shilingi 1,000,000 ambacho hakirudishwi iwapo utaghairi kwenda kwenye shule hiyo. Shule hizo pia nyingine zimeshafungua muhula wao wa masomo, tofauti na utaratibu wa Serikali.

Tatizo lililopo ni kwamba, wazazi tunalazimika kulipa ada kushikilia nafasi kwa hofu ya watoto kupangiwa shule za Serikali zisizokuwa na sifa nzuri katika rekodi zao. Iwapo itatokea mwanao amepata shule ya Serikali yenye sifa, hela yako itakuwa imeliwa kama hutajiunga na shule hiyo ya binafsi. Kwa nini Serikali inakubali utaratibu huu ambapo wananchi wanatapeliwa fedha zao? Serikali pia inaambulia makapi ya wasio na uwezo wa kulipa na au waliochujwamakapi?
 
Peleka malalamiko wizara ya elimu idara ya sekondari au usajili wa shule watakusaidia mkuu pole sana.

Ila kuna agizo lilitolewa kupiga marufuku udahili wa kidato cha tano na vyuo hadi kamishna wa Elimu atakapotoa sifa elekezi....
 
Wao hawapiti hapa kusoma? Pamoja na marufuku hiyo, wanaoendelea kudahili na kufungua shule kabla ya muhula wanafanywa nini?
 
Last week nilikuwa ofisi za NECTA,wamebandika tangazo juu ya suala la usomaj wa ngaz za juu kwa kutumia matokeo haya,wamesema kwamba utaratibu utatolewa na Kamishna wa Elimu,
so mtoa mada subir,maana shule ni july,na shule za binafs wanajua,wanachofanya ni utapeli,ukiangalia yale matokeo ni lazima serikali itoe utaratibu upya,na kama mwanao/mdogo wako amefaulu vizuri ni LAZIMA WAMCHUKUE,NA kuna shule wana utaratibu wa kuwasomesha bure watoto waliofanya vizur sana,
 
Suala nyeti kama hilo unabandika tangazo ukutani? Inatakiwa kutolewa mwongozo magazetini na kwenye TV na kuzuia shule binafsi kufanya udahili kabla ya mwongozo wa Kamishna wa Elimu.
Last week nilikuwa ofisi za NECTA,wamebandika tangazo juu ya suala la usomaj wa ngaz za juu kwa kutumia matokeo haya,wamesema kwamba utaratibu utatolewa na Kamishna wa Elimu,
so mtoa mada subir,maana shule ni july,na shule za binafs wanajua,wanachofanya ni utapeli,ukiangalia yale matokeo ni lazima serikali itoe utaratibu upya,na kama mwanao/mdogo wako amefaulu vizuri ni LAZIMA WAMCHUKUE,NA kuna shule wana utaratibu wa kuwasomesha bure watoto waliofanya vizur sana,
 
Wao hawapiti hapa kusoma? Pamoja na marufuku hiyo, wanaoendelea kudahili na kufungua shule kabla ya muhula wanafanywa nini?

Peleka malalamiko kule si kila mtu anapita hapa kusoma then post yako haina details zote sasa watajuaje?

Mfumo rasmi ni kupeleka kero wizarani...
 
Mkuu, Waheshimiwa wote kabla ya kununua magazeti lazima wapitie hapa JF. Vile vile kuna watu maalum kazi yao ni kupitia karibu mitandao yote ili kuangalia ni kero gani wananchi wanaziibua kila siku!
 
Okay ahsante...

Subiri watakuja kutatua kero zenu hapa hapa....
 
Mbona wengi tu wameweka ufafanuzi katika JF! Tembelea majamvi mengine huko utapata ufafanuzi wa kila jambo na darasa pia. Hujaona watu wanamwaga matokeo mbalimbali humu badala ya kwenda kwenye website husika!
 
Umemwelewa mleta mada?

Analalamika kutozwa 1,000,000 ya kishika uchumba sasa kipi bora? Kumwelekeza sehemu husika anayoweza saidiwa tatizo lake au kumsubiri mkurugenzi wa sekondari aje amsaidie hapa?
 
Suala hili ni la kitaifa, si langu pekee. Sina fursa ya kufika unakoelekeza kutokana na sababu za kijiografia na kiuchumi. Nataka hoja hii ijadiliwe kny forum na hatimaye kuwa public cry, wahusika si lazima walalamikiwe rasmi kwa suala lililo wazi. Govt schools pia zinaathirika kwa kubakiziwa makapi. Ni muhimu kuwa na miongozo yenye adhabu kwa wanaokiuka. Hii ni huduma inayosimamiwa moja kwa Moja na wizara. Si biashara huria kwa kila mtu kujiamulia kivyake.
 
Ahsante wasubiri watakuja.
 
Back
Top Bottom