DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Afya ya Kinywa na Meno kutoka Wizara ya Afya, Dk. Baraka Nzobo amesema kuwa, kulingana na tafiti zilizofanyika, inaonesha kuwa kati ya Watanzania watu wazima, zaidi ya asilimia 76 wanakabiliwa na matatizo ya meno, huku watoto wakikabiliwa na tatizo hilo kwa asilimia 31.
Amesema kuwa changamoto hiyo inachangiwa na mambo mbalimbali, hasa watu wazima kutumia dawa za meno za watoto chini ya miaka mitano ambazo hazina ubora unaolingana na lika la watu wazima.
Amesema kuwa dawa za meno ambazo watu wengi wanatumia ni za watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, ambazo zina kiwango cha madini cha 1000ppm. Hata hivyo, amesisitiza kuwa watu wazima wanatakiwa kutumia dawa za meno zenye kiwango cha 1450–1500ppm.
Ameyasema hayo Machi 26, 2026, katika uzinduzi wa maonesho ya kimataifa ya vifaa na huduma za afya ya kinywa na meno (Tanzania Dental EXPO), ambapo maonesho hayo yatafanyika rasmi Mei 28–30, 2026, katika Jiji la Dar es Salaam.
Aidha, katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, kwa niaba ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amewahimiza wananchi kuzingatia afya zao za kinywa ili kuepuka matatizo.
Naye Mkurugenzi wa Tanzania Dental EXPO, Dr Ambege Mwakatobe, ambao ni waandaji wa maonesho hayo, amesema kuwa yanatarajiwa kuwaleta pamoja washiriki zaidi ya 2,000 kutoka ndani na nje ya nchi, jambo litakalotoa fursa kwa jamii kupata uelewa wa masuala ya afya ya kinywa na meno. Ameeleza kuwa miongoni mwa wadau watakaokuwepo ni taasisi za afya, hospitali, wataalamu binafsi pamoja na watengenezaji wa dawa na vifaa tiba vinavyotumika katika huduma za kinywa na meno.
Vilevile, ametoa wito kwa wadau kujisajili mapema kushiriki maonesho hayo ili kupata fursa zitakazopatikana kupitia maonesho hayo.