Wizara ya Afya: Dalili za corona Tanzania ni tofauti na nchi nyingine

Avriel

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2017
Posts
4,992
Reaction score
5,456
Waziri wa afya asema dalili za corona Tanzania ni tofauti na nchi nyingine duniani, aagiza uchunguzi

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kufanya utafiti kuhusu ugonjwa wa Corona (Covid-19) kwa kuwa kuna tofauti kubwa ya dalili zilizojitokeza kwa wagonjwa hapa nchini ukilinganisha na wagonjwa waliopo nje ya nchi.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipokutana na watafiti wa taasisi hiyo wakati wakijadili maambukizi ya ugonjwa wa Corona na aina ya matibabu ambayo wagonjwa wanatakiwa kupatiwa hasa baada ya kubainika kuwa dalili za ugonjwa huo zinatofautiana na dalili za wagonjwa wa mataifa mengine.

“Kuna mambo mengi ambayo tunapaswa kuyafanyia utafiti wa kisanyansi, moja ni uelewa wa jamii, tunataka kujua wagonjwa wanaougua Corona ni wagonjwa wa namna gani, wana magonjwa ya aina gani, dalili zinazowapata wagonjwa ni za aina gani. Hapa tunataka tupate uwelewa,” amesema Dkt. Ndugulile.

Leo Mei 7, 2020 , amesema kupitia utafiti huo wanataka kujua aina za matibabu ambayo wagonjwa wanatakiwa kupatiwa ili kuhakikisha ugonjwa wa Covid-19 unadhibitiwa hapa nchini.

“Kutokana na muitikio mkubwa wa tiba asili na tiba mbadala, kupitia kikao hiki nawaelekeza wataalamu wetu wajipange kufanya utafiti na kutoa majibu ya tiba ya maambukizi ya virusi vya Corona,” amesema Dkt. Ndugulile.

Amesema wamekubaliana na watafiti hao kufanyia kazi maagizo hayo ndani ya muda mfupi na kutoa majibu sahihi ambayo yatasaidia katika mapambano ya ugonjwa wa Corona.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Yunus Mgaya amesema mapambano dhidi ya ugonjwa Covid-19 ni vita ambayo inapaswa kufanyiwa utafiti ambao utasaidia kupatikana kwa njia sahihi za kukabiliana na maambukizi ya ugponjwa huo.

“Tunafahamu kwamba jamii za kiafrika zina utaalamu katika miti shamba. Katika hili kuna tafiti mbalimbali zinaendelea ili kuchunguza uwezo wa miti shamba kwa lengo la kupunguza makali ya Covid-19.
 
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Yunus Mgaya amesema mapambano dhidi ya ugonjwa Covid-19 ni vita ambayo inapaswa kufanyiwa utafiti ambao utasaidia kupatikana kwa njia sahihi za kukabiliana na maambukizi ya ugponjwa huo.
Sasa hii statement ina uzito gani? DG, we expect more than this simple comment! I might be wrong anyway
 
Hii ya kubanwa mbavu na kuwa na changamoto ya kukosa hewa kufa ghafla NDANI YA SIKU MOJA siyo mojawapo ya symptoms za covid-19 tunazozijua. Inaonekana hii ni dalili tofauti na za WHO! (ie jana alikuwa mzima , leo akabanwa mbavu na kukosa hewa na kufa ghafla).
Kwa kawaida kunakuwa na some hospitalization for some few days kabla ya mtu kufa. Hii ya ghafla ni ya kufanyiwa utafiti. Hii imeripotiwa na vyombo vya habari vingi .....

This needs research if at all if these deaths are due to coronavirus infection
 
Covid19 is real mkuu.
 
I think this should be COVID 20; WHO are working on COVID 19 only.
 
Mpaka sasa corona kasha undergo mutations na kuna aina 3. Yule wa China ni tofauti na wa Marekani na wa Ulayana wa Afrika.

Hata huyu wa Afrika huenda kashajigawanya mara kadhaa na hatujui.
Unforgetable
Japo sio mtaalamu wa Biology ila kwa ulivyosema tu hapo inaonekana huyu wa Africa kama ame mutate alaf akarudi huko Ulayani basi atamaliza vijiji vyote.

Maana si kwa spidi hii anayoenda nayo huku Africa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Yunus Mgaya amesema mapambano dhidi ya ugonjwa Covid-19 ni vita ambayo inapaswa kufanyiwa utafiti ambao utasaidia kupatikana kwa njia sahihi za kukabiliana na maambukizi ya ugponjwa huo.
 
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Yunus Mgaya amesema mapambano dhidi ya ugonjwa Covid-19 ni vita ambayo inapaswa kufanyiwa utafiti ambao utasaidia kupatikana kwa njia sahihi za kukabiliana na maambukizi ya ugponjwa huo.
Hawa wajinga utafiti wao uko wapi?
 
Hii ya kubanwa mbavu na kuwa na changamoto ya kukosa hewa kufa ghafla NDANI YA SIKU MOJA siyo mojawapo ya symptoms za covid-19 tunazozijua. Inaonekana hii ni dalili tofauti na za WHO! (ie jana alikuwa mzima , leo akabanwa mbavu na kukosa hewa na kufa ghafla).
Kwa kawaida kunakuwa na some hospitalization for some few days kabla ya mtu kufa. Hii ya ghafla ni ya kufanyiwa utafiti. Hii imeripotiwa na vyombo vya habari vingi .....

This needs research if at all if these deaths are due to coronavirus infection
Blood clotting blocking lungs-pulimonary embolism
 
Symptoms
Pulmonary embolism symptoms can vary greatly, depending on how much of your lung is involved, the size of the clots, and whether you have underlying lung or heart disease.

Common signs and symptoms include:

Shortness of breath. This symptom typically appears suddenly and always gets worse with exertion.
Chest pain. You may feel like you're having a heart attack. The pain is often sharp and felt when you breathe in deeply, often stopping you from being able to take a deep breath. It can also be felt when you cough, bend or stoop.
Cough. The cough may produce bloody or blood-streaked sputum
 
Ngoja twende kwa jiwe kwanza
kobekatuni-20200508-0001.jpg
 
Inaonekana wataalamu wetu wapo nyuma sana, hizo sudden deaths, zinaletwa na blood clots kwenye lungs, mapafu, wengine wanapata strokes, baada ya clots kufikia organs zingine, sasa sisi tusio wataalam tunausoma huu ugonjwa kutoka mitandaoni kwa mabeberu huko, wao wanashindwa??

Ukistaajabu ya firauni utayaona ya COVID Danganyika...

Everyday is Saturday....................... 😎
 
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Yunus Mgaya amesema mapambano dhidi ya ugonjwa Covid-19 ni vita ambayo inapaswa kufanyiwa utafiti ambao utasaidia kupatikana kwa njia sahihi za kukabiliana na maambukizi ya ugponjwa huo.

Juhudi za kutokomeza Corona tukizibrand ‘VITA’ tayari tumechagua fungu la kushindwa. Na ni hulka ya siasa kutumia neno ‘vita’. Mfano tuna vita nyingi tu zimeshatushinda, vita ya umasikini, vita ya madawa ya kulevya, vita dhidi ukeketaji. Ni neno la kisiasa linaloashiria ukosefu wa uwajibikaji.
 
Back
Top Bottom