Wizara ya Afya: Dalili za corona Tanzania ni tofauti na nchi nyingine

mkuu hakuna mgonjwa wa corona anyekufa ghafla ni kwamba amepata maambukizi na hakupimwa mapema ili apatiwe msaada wa kimatibabu, mtu anazidiwa na ugonjwa hivyo akipelekwa hospitali kwa matibabu inakuwa too late anakufa ndo hii wanaiita kufa ghafla.
Haya yalijitokeza hata kule China siku za mwanzoni watu walikuwa wanaanguka barabarani kwa kukosa pumzi na akikimbizwa hospitali hachukui round anakufa.
 
Hatari sana hii mkuu...
 
Nakubalina na maelezo yako! Ilianza kunipa mashaka kuwa mbona watu wanalazwa for some days? How come hapa mtu anaanguka ghafla wakati jana alikuwa mzima wa afya tele?
 
Mimi nafikiri ni yale yale kama ya chattle, watu wako incompetent, hawataki kufuata kanunu za WHO na sasa wanatafuta visingizio vya kila aina...eti dalili za corona Tz ni tofauti na nchi nyingine...na ndio maana kuna corona hadi kwenye mapapai. Kuna tatizo la kiweledi!
 
Kama uliona ile clip ya nesi wa Marekanj alisema Blacks wanakufa kwa wingi kwa sababu Corona inakuja kama mild kumbe ndani mapafu yanashambuliwa,
so akija kubanwa inaweza kuwa less than 20mnts anaondoka
 
Walichotakiwa kujua toka mwanzo Corona ni hatari saana Nchi zote hizo wapo wagonjwa walikua wanasondoka huku wakiwa njiani ni vile wataalamu wapo busy kuwasikiliza wanasiasa...
 
Kama uliona ile clip ya nesi wa Marekanj alisema Blacks wanakufa kwa wingi kwa sababu Corona inakuja kama mild kumbe ndani mapafu yanashambuliwa,
so akija kubanwa inaweza kuwa less than 20mnts anaondoka
asante, clip sijaiona. Ila sasa napata mwanga mkubwa.
 
Nakubalina na maelezo yako! Ilianza kunipa mashaka kuwa mbona watu wanalazwa for some days? How come hapa mtu anaanguka ghafla wakati jana alikuwa mzima wa afya tele?
tatizo kubwa la mashambulizi ya covid 19 virus ni kupelekea kitu kinaitwa BLOOD CLOTS kwenye mapafu (pulmonary embolism ), hii ni kama mabonge ya damu (makubwa/madogo) ambayo yanajazana taratibu bila mtu kujua na yakijaa basi vitundu hewa vinaziba ndo hiyo mtu anakosa pumzi na kupelekea kifo ndani ya muda mfupi.
Mbaya zaidi ni kwamba watu weusi wengi/Africans hatuoneshi dalili mapema kama ilivyo kwa jamii za wenzetu caucasians na hao mongols.
 
Ni kweli kabisa.
Watu wanaumwa leo kesho anakufa. Tofauti na uraya
 
Hawa wadudu ni kama "kanitangaze",

Wanataka wakifika sehemu muwaseme kwa jina lao, mkiwa puuza au kuwabatiza majina mengine lazima waongeze dosage. Sehemu zote walikopokelewa kwa kupuuzwa wameacha makovu ambayo hayatasahaulika.

Tukubali hali ni tete na wananchi wajue ili kila mmoja pamoja na hatua zinazoainishwa na wizara, wachukue hatua mahususi kuwaepusha na covid-19.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kichwa cha habari kinashabiiana na vichwa vya habari vya magazeti ya udaku

Upuuzi ⚰️
 
G.Jacob hata mimi ningependa kila baada ya siku 14 niwe najipima; hiyo huduma ya vipimo inapatikana wapi kwa Arusha?
 
G.Jacob hata mimi ningependa kila baada ya siku 14 niwe najipima; hiyo huduma ya vipimo inapatikana wapi kwa Arusha?
Tena kama humu Arusha ndio mtihani kabisa sidhani hata kama kuwapima wagonjwa ni kipaumbele chao, halafu nasikia ni bei ghali kwa kipimo hiki hata mimi ningeenda kupima
 
G.Jacob hata mimi ningependa kila baada ya siku 14 niwe najipima; hiyo huduma ya vipimo inapatikana wapi kwa Arusha?
hakuna hospitali yenye vipimo vya covid hadi sasa ni maabara kuu ya Taifa pekee kwa hapa Tanzania ndio maana ukienda utachukuliwa sampuli zako na kutumwa Maabara ambayo ipo Dar....kisha utasubiri majibu yako hadi yatakapotoka, hivyo fika kituo cha afya i.e hospitali ya wilaya ulipo wakuchukue sampuli zako kwa vipimo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…