PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Wizara ya Afya imetoa taarifa muhimu kwa umma kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa Ebola unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), pamoja na kugundulika kwa mgonjwa nchini Kenya aliyesafiri kutoka DRC. Hata hivyo, Wizara imesisitiza kuwa hadi sasa hakuna ugonjwa wa Ebola uliothibitishwa nchini Tanzania.
Wizara imewataka wananchi kuzingatia hatua za kujikinga, ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kuepuka kugusa majimaji ya mwili wa mtu mwenye dalili zinazofanana na Ebola au aliyefariki kwa dalili hizo, pamoja na kuepuka kugusa wanyama pori kama popo na sokwe. Wananchi pia wametakiwa kutoa taarifa kwa kupiga simu bila malipo kupitia namba 199 wanapobaini mtu mwenye dalili zinazofanana na ugonjwa huo.
Aidha, Serikali inaendelea kuimarisha ufuatiliaji wa afya katika viwanja vya ndege, bandari na mipaka ya nchi, huku ikiwataka wahudumu wa afya kuzingatia kanuni za kuzuia na kudhibiti maambukizi. Wizara imewahimiza wananchi kufuatilia taarifa kutoka vyanzo rasmi vya Serikali ili kupata taarifa sahihi na kuepuka upotoshaji kuhusu ugonjwa huo.
Soma pia

- Visa vya Ebola Kenya vyafikia 8, Muhudumu wa Hospitali ya Nairobi aambukizwa
- Kenya yathibitisha Visa vipya 4 vya Ebola. Jumla ya Wagonjwa yafikia 7
- Kenya yathibitisha kisa cha kwanza cha Mgonjwa wa Ebola – Mgonjwa Mkenya amefariki
- Tanzania yaimarisha ukaguzi wa Ebola mipakani, Wasafiri wanaotoka maeneo hatari kufuatiliwa kwa siku 21
- Wizara ya Afya yatoa mwongozo wa jinsi Ebola inavyoenea na hatua za kujikinga