Wizara ya Afya ikemee hawa madaktari feki wa mitandaoni wanaotoa shauri za kiafya zisizofaa

Wewe mkewe ungesaidia kufafanua allichopost mumeo
 
Mganga mkuu wa serikali, Dr.Grace atawashughulikia. Mpe taarifa huwa hamung'unyi maneno.
 
Mitandaoni kuna fujo kuna makungwi ambao ndoa zimewashindwa,kuna wale washauri wa mapenzi ambao nao wanachwa kila siku, kuna washauri wa chakula hawajui hivyo vyakula vina vitu gani ndani,kwenye walimu wa mazoezi ndio usiseme wao wanashika misambwanda ya wake za watu watu na hawana wanacho kijua kuhusiana na mazoezi. Halafu kuna hao washauri wa Afya na wengi naona wamejikita kwenye afya ya akili, ukiwasikiliza ndipo unapojua wao ndio wenye hilo tatizo.

Halafu kuna wachambuzi mpira wa miguu ndio usiseme.
 
Ungemwambia huyo "Ommy" akupeni maelezo ya kila dondoo kwa kina na faida zake kwa mshauriwa.
NB;Utandawazi umeekuja na utakuja na mengi mchanganyiko.Ni juu ya mlaji kutumia akili zaidi kuliko kupaniki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…