Wizara ya Afya imekosa viongozi waadilifu hadi kuteua wenye tuhuma nzito za ufisadi?

Wizara ya Afya imekosa viongozi waadilifu hadi kuteua wenye tuhuma nzito za ufisadi?

Mapundam

New Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
4
Reaction score
1
Wizara ya Afya imekosa viongozi waadilifu hadi kuteua wenye tuhuma nzito za ufisadi?

Kupitia jukwaa hili la JamiiForums, tunapenda kuhoji na kuomba ufafanuzi wa wazi kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Afya pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhusu muendelezo wa teuzi zinazoacha maswali mengi kuliko majibu katika sekta yetu ya afya.

Mfano hai unaochochea taharuki na maswali kwa sasa ni uteuzi na nafasi anayoishikilia Dr. Deogratias Banuba kama Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, akitokea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida. Tunaiomba Wizara na vyombo vya uchunguzi vitujibu maswali haya ya kiraia:

Maswali Muhimu kwa Wizara ya Afya:

  • Je, Wizara imekosa kabisa watendaji waadilifu na wasio na madoa hadi kuendelea kumshikilia kiongozi anayekabiliwa na tuhuma nzito za ubadhirifu wa zaidi ya Shilingi Milioni 260 za mradi wa ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto (Maternity Building) wakati akiwa Singida? Hadi sasa jengo hili halijakamilika kama lilivyokusudiwa kwa ajili ya kuhudumia wananchi.
  • Inakuwaje mtumishi ambaye kesi yake ipo mahakamani na hivi karibuni tu tarehe 8/7/2026 alikuwa na muendelezo wa shauri lake bado anapewa dhamana kubwa ya kusimamia rasilimali na mali za umma Katavi? Je, taratibu za utumishi wa umma hazitaki mtumishi kusimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma kama hizi?
  • Je, ukimya huu unamaanisha Wizara inabariki uwepo wa viongozi wenye tuhuma mahakamani kuendelea kuongoza hospitali zetu?
Maswali kwa TAKUKURU (Mkoa wa Singida):

  • Vyanzo vyetu vinaashiria kuwa mtuhumiwa alikamatwa na kuwekwa ndani hivi karibuni, lakini kukawa na mchango wa dharura kutoka kwa Waganga Wafawidhi wenzake ili kufanikisha kuachiwa kwake. Je, TAKUKURU Mkoa wa Singida hamuoni viashiria hivi vya uwepo wa mtandao unaolindana kimaslahi?
  • Ni hatua gani thabiti zinachukuliwa kuhakikisha kuwa fedha za ujenzi zilizopotea Singida zinarudi na kwamba haki haipindishwi mchana kweupe ili akinamama na watoto wapate huduma inayostahiki?
Wito

Sekta ya afya inagusa maisha ya wananchi wanyonge kila siku. Tunaiomba Wizara ya Afya na mamlaka zote za nidhamu kutoa kauli na kuchukua hatua stahiki ili kurejesha imani ya wananchi. Kodi na rasilimali zetu hazipaswi kuwa mtaji wa kulinda au kumpasisha kiongozi yeyote anayetuhumiwa kwa ufisadi.

Tunasubiri majibu na hatua za kiutawala na kisheria.
 
Kwani masisiemu walifanya nini tofauti hadi hii iwe spesheli?
 
Wizara ya Yule jamaa aliesifiwa na nyoka kishungi kuwa anakifua kipana
 
Back
Top Bottom