Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 25,725
- 78,589
Usalama wa Taifa ni pamoja na Utulivu wa Raia wake.
Kiukweli kabisa Huwa Nashangaa hii Nchi yetu vipi?
Trump kajitoa WHO, taarifa na vumi mbalimbali kuhusiana na upatikanaji wa ARVs zinazunguka kwenye mitandao ya kijamii kila kukicha, lakini HUSIKII serikali ikichukua hatua kuongea na vyombo vya habari ili kuleta utulivu kwenye jamii.
Pia soma: Rais Trump amesaini amri ya kuiondoa Marekani kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
Yaan hii Nchi kila kitu kinachukuliwa poa tu, hapo suala nyeti kama hili linachukuliwa tu kama ni stori za mitandaoni za udaku, basi.!
Tafasiri yake ni nini? Serikali imeacha mwanya ambao wahuni, watumishi wezi wasokua na Uadilifu kutengeneza "UKOSEFU HEWA" wa Dawa za ARV, hali inayoenda kuzalisha Vita kubwa ya upatikanaji wa dawa hizo kwa watumiaji.
Watumiaji wa ARV ni wazi sasa wanaenda kuingia kwenye mashindano ya kupata, hali hii inaenda kufanya WENYE HELA KUPATA DAWA HIZO NA KUJITUNZIA ZA ZIADA huku Masikin wakiambiwa "Dawa hazipo, Trump kasitisha".
Chonde chonde Serikali, Usalama wa Taifa, TAKUKURU, Hakikisheni mnaleta utulivu kwa jamii, kila mmoja aiingie kazini rasmi.
Ndugu zangu watumiaji wa ARV's, Dawa zipo za Kutosha, Usikubali MTU akutengenezee mazingira ya kuzinunua.
ARV haziuzwi ni Bure.
Watumiaji wa ARV bila kujali hali zao za kiuchumi wote wanahaki ya kupata ARV.
Naona ongezeko kubwa la Maambukizi ya VVU.
Naona vifo vingi ambavyo si tu vitahusiana na UKIMWI, la hashaaa, vitahusiana na watu kutokua na taarifa sahihi sambamba na hili janga hewa litakaloletwa na watumishi wasokua na maadili.
Wizara ya Afya Tanzania
=====
Pia soma: Wizara ya Afya yatoa ufafanuzi kuhusu upatikanaji wa ARV, wasema zipo za kutosha