Wizara ya Afya mtuangalie upya wanataaluma wa Maabara za Binadamu

Lukumbisi

Senior Member
Joined
Jan 28, 2022
Posts
110
Reaction score
188
Habari wana Jf.

Nimeona nilete mbele ya jukwaa hili jambo ambalo kimsingi linatesa sana kada hii ya afya yaan Medical lab personels.

1. Kuwepo kwa Provisional license ya maabara. Yaani ikiwa mtu amehitimu na amequalify kabisa kwanini unampa leseni ya matazamio? Unamtazama huyu mtaalamu akiwa wapi ikiwa nyie serikali hamtoi ajira kwa watu wenye leseni za awali? Na vituo binafsi pia ndo wamepata sababu za kulipa ujira mdogo et kisa una leseni ya awali.

Jaman hili jambo linatuumiza sana. Hiyo ni tofauti kabisa na kada nyinginezo za afya mfano famasia, nurses na madaktari ambapo wenzetu wanapata full registration yaani hana muda wa kusubiri leseni ya nyingine manesi nao ni hivohivo sijajua kwa kada nyinginezo, why Labs?

2. Kufelishana mitihani kwa makusudi, taaluma nakuta kuna baadhi ya vituo vya kufanyia hiyo mitihani ya leseni za maabara watu wanakimbia kwa kuwa kuna mambo ya ajabu hasa hapo Muhimbili mna mambo ya hovyo sana.

Yaani unajisikiaje kusapisha mtu ili upate pesa yake ya sup inakusaidia nini laki moja ya kijana fukara kajitafutia hela kwa taabu.

Mwisho niseme tu kuwa najua humo pia mpo wahusika wa taaluma hii mkalifanyie kazi msifanye mambo kuwa magumu, ugumu tulioupata kwenye ANATOMY PHYSIOLOGY NA BIOCHEMISTRY UNATOSHA.

Mtupumzishe basi.
 
Habari wana Jf.

Nimeona nilete mbele ya jukwaa hili jambo ambalo kimsingi linatesa sana kada hii ya afya yaan Medical lab personels.

NIsiache kukupa pole. Ukweli mchungu: "akuangalie nani, mlamba asali?" Labda tu kama umesahau:

"Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe."

Hebu fanyeni kama mnajikuna, muone kama mtakuja tena huku kulilia kama vifaranga vya kuku wa kisasa.
 
Kama watu wamefundishwa na kuhitimu, leseni ya majaribio ni kwa ajili ya nini? Haya haya mambo ndo yamefanywa kwa madaktari wa mifugo walikuwa wanalalamika kunyimwa usajili hadi wafanye internship mwaka mzima na serikali haitaki kuwalipia, kwa nini mnawapa usumbufu hawa vijana hadi waione nchi yao chungu?​
 

Ninakazia: "Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe."

Huku kwingine awasikie nani?
 
Hili baraza litakuwa na watu wa hovyo hovyo tu,wanawapa Provisional halafu wanarudi mtaani wanasema mtaalamu mwenye Provisional haruhusiwi kufanya Kazi maabara mpaka awe na Full registration.Sasa hata hio Provisional ina kazi gani?

Ni kwamba wanatengeneza usumbufu usio na lazima kwa wanataalumu na wamiliki maana wakikuta huyu mtaalamu mwenye Provisional mmiliki nae anapigwa fine.
 
Nyie ndo mwasababisha watu wanapata usugu
 
Kwel mkuu umeongea point kabisa yaan hyo mitihani unafelishwa mpaka basi utakuta MTU umetoka katika familia yenye maisha magumu umepamban kwa aina zote umepata hyo laki na nusu unaenda fanya mtihan lakn wanakufelish kusud ili urudie tena uwape hela inauma sana
 
wenzenu mawakili wanalipa ada more than 1.5 M Na wanafaulu 20 kati ya 600
 
Sawa hata analyelipa iyo laki n nusu pia anapata maumivu ujui katoka familiya yenye kipato gani na
 
Nani akuonee huruma wewe mama samia ?? Au mwigulu nchemba au philip mipango au ndalichako nauliza tena nani wa kukuonea huruma wewe πŸ€”πŸ€”πŸ€” nakushauri sana komaaa....utakapofikisha umri wa miaka 40 watu watataka waone maendeleo na hiyo elimu uliyonayo wala haitakuwa na maana yoyote hata ungekuwa na phd 100 😁😁😁😁 ohooooooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…