Wizara ya Afya na dawa za GNLD, Forever Living

Wizara ya Afya na dawa za GNLD, Forever Living

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Nguvu kubwa ya kichinichini inatumika kutangaza dawa za makampuni mbalimbali yanayouza dawa za tiba mbadala kwa bei ya juu sana zisizo na maelezo ya kina kutoka serikalini kuhusu ubora na uhalali wa dawa hizo. Zinasambazwa chinichini mithili ya DECI na UPATU.

Watu wa AFYA tafadhali tuambieni sisi wananchi kuhusu ubora, usalama na gharama halisi za dawa hizi kabla sijajiunga na mtandao huo. Kwasasa zizijua bidhaa za GNLD, Forever Living, na Eternal.
 
hao ETERNAL BALAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
 
Wenyewe hawaiti DAWA wanasema ni FOOD SUPPLEMENTS.
 
Wale ni wezi na sisi mwanaume ukifika pale kupima lazima uambiwe una tezi dume ss nenda kwenye dawa sasa utachoka utaambiwa tumia dawa mara kuna dawa toka nairobi kwanza kama hawa watu wanataaruma
 
Wao huwezi kuwabana bse hawauzi dawa kama alivyosema mdau mwingine hapo juu ni virutubisho. Ss utakuta kama ni virutubisho wameoimiwa na TBS na vikakidhi ubora wa virutubisho. Sema changamoto kwa members wao wasiopenda kujifunza ndo wakija wana maneno kama cherehani ya umeme kiasi chankukushawishi zile ni dawa japo zinasaidia sana kwa baadhi ya watu
 
Hakuna dawa zaidi ya Chakula halisi kula karoti,vichwa vya samaki,dona,matunda,mbogamboga zisiive sana.Hao matapeli na kodi hawalipi
 
Wale ni wezi na sisi mwanaume ukifika pale kupima lazima uambiwe una tezi dume ss nenda kwenye dawa sasa utachoka utaambiwa tumia dawa mara kuna dawa toka nairobi kwanza kama hawa watu wanataaruma
serikali inakosa kodi kizembe kutoka kwa hawa mabwana na kusababisha wananchi kuuziwa visanvu kwa bei kubwa sana.
 
Back
Top Bottom