Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Wakuu kwa wenye uzoefu, je ni sahihi DMO kua Nurse mwenye Diploma (RN)?, uku wilaya ya Nkasi tuna sitofaham hyo kwa sasa. DMO kaenda kusoma aliemkaimisha nafasi ni RN na wilaya ina watu wenye sifa za kushika hyo nafasi.
Punguza uchawi, sisi....
1. PMU wetu ana diploma na anaowaongoza wana bachelor
2. Afisa biashara ana degree na anaowaongoza wana Masters
3. DT ana bachelor bila CPA ila anaowaongoza wana CPA.

Punguza UCHAWI.

#YNWA
 
  • Thanks
Reactions: apk
Hivi kwanini watumishi wapya wanalipwa malimbikizo ya mishahara chapu chapu huku wale waliopo kazini miaka kadhaa kila mwaka tunaambiwa tujaze Fomu?
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Wizara kama wizara. Hongereni kwa kazi. Hongera Katibu kwa kazi. Yangu machache. Nimekuwa na proposal fulani ambayo nilishafika hadi wizarani kipindi hicho ipo Dar. Wahusika pale danadana zikawa nyingi na hatimaye sikuweza kufanikisha jambo langu. Ningetamani sana kukutana na Katibu wa wizara ndugu Dr. Jingu ili aweze kuyasikia mapendekezo yangu tuone namna ya kufanya. Bila shaka uzi huu hauko hapa kwa bahati mbaya.
 
Habari hapo wizarani, npenda kuelewa kwa kina ni kwa namna gani wizara hii nyeti inasimamia dawa nyingi zinazotangazwa na kuuzwa mitandaoni, maana sioni alama yenu yoyote kwamba imesajiliwa na ni salama ka matumizi ya binadamu lakini pia inatibu kwa usahihi kile kinachosemwa. vinginevyo hilo bomu hatari kabisa.
Ahsante
 
Watumishi wenu wa afya kituo cha amana ndogo pale kivule hawapo serious na kazi kabisa, mwaka jana tumepata hasara ya kuwa na mtoto ambaye ana magonjwa mengi kuliko umri wake.

Imagine mke wangu anafika kujifungua kuanzia asubuhi mpaka jioni madaktari hawapo anajifungua usiku wa manane kwa massada wa wauguzi tu na madaktari wa zamu hawakupokea simu mpaka anakuja mmoja asubuhi mtoto amepata shida hakulia wanashindwa kumpa rufaa aende amana referal wanamuweka mpaka daktari afike.

Sasa huyu mtoto asipokaa sawa kama ninavyomtumania basi nitawapiga majini kituo kizima hapo.😡😡😡
 
Kuna kipindi nilikuwa na mgonjwa hospitali ya umma ya Wilaya, akatakiwa ahamishiwe hospitali ya mkoa (ya rufaa), niliomba Ambulance ya kutoa mgonjwa kumpeleka hospitali ya Rufaa umbali wa kama kms 15.
kwa sababu hospitali ilikuwa karibu, nikaomba kama hawana waombe itoke kule hospitali ya Rufaa kwani nitachangia..
Nikajibiwa kuwa, zile Ambulance ninazo ziona kule Hospitali ya mkoa ni kwa ajili ya huduma ya mama na mtoto tu....Huwezi kuamini ilibidi nipeleke mgonjwa kwa kutumia gari ya private.
Naomba muongozo wa kupata Ambulance ukiwa hospitali za ngazi ya wilaya....kwani inaoneka huku chini (ngazi ya vituo vya Afya) wanatoa ushirikiano kuliko huku juu....
 
Matibabu ongezeni madaktari ili kupunguza foleni muende na muda watu watibiwe haraka

Mtu kama hana pesa ya matibabu atibiwe haraka na awekewe u taratibu waa wakulipa polepole

Gharama za matibabu zipunguzwe tafadhali

Dawa zipatikane kwa wingi
Hili wazo la muimu sana afya ipewe kipaumbele sana, matibabu kwa mda na uraisi wa kupata huduma pia kipaumbele itolewe kwa wazee, wajawazito, watoto na wagonjwa wa dharula (emergency)
 
Condom za Sasa hivi zimechakachuliwa
Unaweza kuta ukiwa katika jitihada za kuivaa tu mara unashangaa imepasuka Kuna jitihada zozote mlizochukua kulitokomeza hilo?
Usivae kama ugomvi. Valishwa na mwenza wako haitachanika
 
Kuna kipindi nilikuwa na mgonjwa hospitali ya umma ya Wilaya, akatakiwa ahamishiwe hospitali ya mkoa (ya rufaa), niliomba Ambulance ya kutoa mgonjwa kumpeleka hospitali ya Rufaa umbali wa kama kms 15.
kwa sababu hospitali ilikuwa karibu, nikaomba kama hawana waombe itoke kule hospitali ya Rufaa kwani nitachangia..
Nikajibiwa kuwa, zile Ambulance ninazo ziona kule Hospitali ya mkoa ni kwa ajili ya huduma ya mama na mtoto tu....Huwezi kuamini ilibidi nipeleke mgonjwa kwa kutumia gari ya private.
Naomba muongozo wa kupata Ambulance ukiwa hospitali za ngazi ya wilaya....kwani inaoneka huku chini (ngazi ya vituo vya Afya) wanatoa ushirikiano kuliko huku juu....
Sasa huyo waziri wa kulishuhulikia hili umemuona wapi?
 
Wizara ya afya kitazameni chuo Cha Tabora EA polytechnic kwa karibu,
Wanafunzi wananyimwa kufanya mitihani kisa semester ya kwanza tu kisa kutokamilisha malipo ya ada hata kwa kiasi kidogo Cha elfu mbili au Tano kinachobaki, hii nimesikia wakilalamika kwamba Wana mitihani 24/2/2025 na wamenyimwa fursa hiyo hasa waliopo mwaka wa 2&3
 
Wizara yoyote anayohudumu Jenister haina maajabu. Nivurugu tu
 
Sijui kama bado mnafuatilia hili jukwaa
Ila niseme tu hao ma itern mnapeleka huko Hospitali za Rufaa wanatoka Sifuri
Inamaana mkiwapeleka huko kuwapa Hospitali ndio wana anza kufanya practical
Nasema hivyo kwa sababu Nilikuwa na mgonjwa Hospitali ya Rufaa Ma intern wana hamishwa kila siku tatu fikiria kule wagonjwa wapo serious ...Intern anatoa dawa ndani ya siku tatu na hazija respond... amesha hamishwa (kwa hiyo hapo ametoka sifuri)
Anakuja intern mwingine dawa zinabadilisha (Zikimsaidia mgonjwa anabahati tofauti na hapo na yeye anahamishwa) yaani kwa mtu mwenye Elimu kiasi anaona wale wapo pale kama wanazurura tuu...
Watoto wa watu wapo very dedicated ila hawasaidiwi...wana achiwa kila kitu wakati wanahitaji msaada.
Hawapati muda wa kuwa karibu na mgonjwa na kuweza kumfuatilia...
na hao wanaojiita madactari Bingwa ndio hawaonekani...hardly dakika 4 - 10 kama una bahati kwa mgonjwa ambaye hata tatizo halijafahamika ....yaani hatupo serious na maisha ya watu.....
 
Sijui kama bado mnafuatilia hili jukwaa
Ila niseme tu hao ma itern mnapeleka huko Hospitali za Rufaa wanatoka Sifuri
Inamaana mkiwapeleka huko kuwapa Hospitali ndio wana anza kufanya practical
Nasema hivyo kwa sababu Nilikuwa na mgonjwa Hospitali ya Rufaa Ma intern wana hamishwa kila siku tatu fikiria kule wagonjwa wapo serious ...Intern anatoa dawa ndani ya siku tatu na hazija respond... amesha hamishwa
Sasa anakuja intern mwingine dawa zinabadilisha yaani kwa mtu mwenye Elimu kiasi anaona wale wapo pale kama wanazurura tuu...
Majaribio kwenye afya za watu
 
Back
Top Bottom