Wizara ya Afya Tanzania angalieni upya Sera za Chama cha Madaktari (MCT)

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
8,406
Reaction score
9,619
Wakuu jf kila mmoja kwa imani yake namsalimia.

Leo niko na Wizara ya Afya kama nguzo ya kusimamia taasisi zilizo chini yake mfano chama cha Madactari (MCT).

Kwa nini ichi chama kimekua na ukiritimba wa kipumbavu kwa vijana wetu, ambao serikali wengine imewagharamikia, na wengine ndugu/ wazazi wamepambana kulipa mapesa mengi ili vijana wao/ ndugu zao watimize ndoto zao walizozitaka?

Wizara ya afya ni serikali, na ijulikane sio product zote zinazalishwa ipo na uwezo wa kuziajiri. Kama ndivyo kumbe wengine wataajirika na wengine kujiajiri na vyoyote vile serikali itapa kodi.

Kwa mantiki hii hiki chama kupitia wizara husika kigugumizi kinatoka wapi kuwapatia leseni bure ili hali hizo leseni hulipia kila mwaka wachukuapo kila mwaka? Huu ni upumbavu mkubwa.

Leo zipo mada nyingi zikimzungumzia Dkt. Janabi why awe na jina kubwa ilihali hakupitia ujinga/ukiritimba wa namna hii?

Serikali imedhamini vijana wengi tu kupitia bodi ya mikopo hizo pesa zinarudishwaje kama hizi product walizo zilipia mapesa mengi zimefungwa mikono?

Mbunge Kishimba amewahi toa hoja bungeni kwamba kama Masai anaweza tembeza na kuuza dawa mbalimbali na wala hapati shida toka kwa mamlaka, inakuaje kijana ambae amekaa darasani miaka 5, intern miaka 1, jumla miaka sita ashindwe hata kutoa huduma kwa jamii inayo mzunguka? Wabunge nafikiri hawakumuelewa vizuri!

Waziri wa afya unayo nafasi, Rais unayo nafasi ya kuweka hili jambo sawa, yaani serikali inafanya jitihada kwamba vijana watimize ndoto zao na mwisho wa siku inawanyongelea mbali wale ambao imewahudumia kama sio kutengeneza chuki kwa serikali pitia hivi vyama uchwara nini?

J. Mhagama (MP na waziri) chukua hili na lifanyie kazi sina shaka na wewe.

Thanks, by 4 7mbatizaji
 
Ni kweli kuna huo utaratibu ambao ulianza 2019/2020 ambapo wote wanaohitimu miaka mitano ya udaktari hufanya mtihani kutoka MCT kabla ya kuanza mafunzo ya utarajali (internship) ya mwaka mmoja. Pia baada ya kumaliza mafunzo hayo (internship) kuna mtihani mwingine ambapo daktari akifaulu atapewa leseni yake ya udaktari na asipofaulu basi atalazimika kusubiri mtihani mwingine, mpaka afaulu.

Baraza, MCT walidai kwamba lengo la mitihani hiyo ni kusaidia kuwapata madaktari mahiri. Pia kulikuwa na hoja kwamba mitihani kama hiyo inafanyika katika nchi zingine kama UK, Canada, nk.

Hata hivyo mitihani hiyo imekuwa na athari mbaya hasa kwa wale ambao wanapata matokeo mabaya kwani hawawezi kupata leseni zao hivyo kusota mtaani bila kufanya kazi ya udaktari. Unakuta nafasi za kazi zinatoka mfano hospital za binafsi lakini wanakosa kwa sababu ya kukosa leseni.

Naamini kuna umuhimu pia wa baraza la madaktari, MCT kufanya tathmini ya matokeo ya mitihani hiyo ili kuona kama malengo mahususi ya mitihani hiyo zimefikiwa na kwa kiwango gani.
 
Eti form four aliyesoma ADO anaruhusiwa kuuza dawa kwenye DLDM ila nurse aliyehudumu pharmacy za vituo vya afya na hosp haruhusiwi mpaka akasome ADO.
 
Je chaguo la A,B,C, D ndo kipimo halisi cha vijana hawa , mbona alama za ABC D zaweza kubetiwa tu , acheni upumbavu , kama ndivyo kwa nini msije na mtazamo mwingine kwamba kijana kabla ya kumaliza intern aje ana andiko mahalum kuliko ujinga huu
 
Mkuu ndiyo maana nikasema kwamba baraza la madaktari Tangayika (MCT) ni vyema wakafanya tathmini ya hicho wanachofanya kama kweli kinazalisha madaktari mahiri au ipo tu!?

Kwa hayo hayo malengo waliojiwekea kwamba mitihani hiyo itawafanya wao wapate madaktari mahiri basi waangalie kama yamefikiwa.
 
Eti form four aliyesoma ADO anaruhusiwa kuuza dawa kwenye DLDM ila nurse aliyehudumu pharmacy za vituo vya afya na hosp haruhusiwi mpaka akasome ADO.
Upumbavu mkubwa, sawa na dr amesoma jumla ya miaka 6 alafu eti chama uchwara ,kinampa mtiani wa ABCD wakuchagua ili kupima uwezo wake kama sio utahira ni nini
 
Nomaa sanaa ili mradi utesekee tuu
 
Ni kweli kuna huo utaratibu ambao ulianza 2019/2020 ambapo wote wanaohitimu miaka mitano ya udaktari hufanya mtihani kutoka MCT kabla ya kuanza mafunzo ya utarajali (internship) ya mwaka mmoja. Pia baada ya kumaliza mafunzo hayo (internship) kuna mtihani mwingine ambapo daktari akifaulu atapewa leseni yake ya udaktari na asipofaulu basi atalazimika kusubiri mtihani mwingine, mpaka afaulu.

Baraza, MCT walidai kwamba lengo la mitihani hiyo ni kusaidia kuwapata madaktari mahiri. Pia kulikuwa na hoja kwamba mitihani kama hiyo inafanyika katika nchi zingine kama UK, Canada, nk.

Hata hivyo mitihani hiyo imekuwa na athari mbaya hasa kwa wale ambao wanapata matokeo mabaya kwani hawawezi kupata leseni zao hivyo kusota mtaani bila kufanya kazi ya udaktari. Unakuta nafasi za kazi zinatoka mfano hospital za binafsi lakini wanakosa kwa sababu ya kukosa leseni.

Naamini kuna umuhimu pia wa baraza la madaktari, MCT kufanya tathmini ya matokeo ya mitihani hiyo ili kuona kama malengo mahususi ya mitihani hiyo zimefikiwa na kwa kiwango gani.
Mitihani ni lazima Ili mtu ahakikiwe kweli anaweza kupatia watu matibabu sawa sawa. Afya za watu si kitu Cha mchezo.
Mitihani ya madaktari ni nchi nyingi sana ipo.
 
Mkuu ndiyo maana nikasema kwamba baraza la madaktari Tangayika (MCT) ni vyema wakafanya tathmini ya hicho wanachofanya kama kweli kinazalisha madaktari mahiri au ipo tu!?

Kwa hayo hayo malengo waliojiwekea kwamba mitihani hiyo itawafanya wao wapate madaktari mahiri basi waangalie kama yamefikiwa.
Nimekuelewa mkuu ,

Mfano ukiwekewa swali mzazi unamtabuaje kwako.
A.anae kulea
B. anae kusindikiza shuleni
C. anae kununulia nguo kila siku

Jibu lolote utatoa katika ABC wenda ukipatia lisikusaidie popote mkuu
 
Wakuu jf kila mmoja kwa imani yake namsalimia.

Leo niko na Wizara ya Afya kama nguzo ya kusimamia taasisi zilizo chini yake mfano chama cha Madactari (MCT).

Kwa nini ichi chama kimekua na ukiritimba wa kipumbavu kwa vijana wetu, ambao serikali wengine imewagharamikia, na wengine ndugu/ wazazi wamepambana kulipa mapesa mengi ili vijana wao/ ndugu zao watimize ndoto zao walizozitaka?

Wizara ya afya ni serikali, na ijulikane sio product zote zinazalishwa ipo na uwezo wa kuziajiri. Kama ndivyo kumbe wengine wataajirika na wengine kujiajiri na vyoyote vile serikali itapa kodi.

Kwa mantiki hii hiki chama kupitia wizara husika kigugumizi kinatoka wapi kuwapatia leseni bure ili hali hizo leseni hulipia kila mwaka wachukuapo kila mwaka? Huu ni upumbavu mkubwa.

Leo zipo mada nyingi zikimzungumzia Dkt. Janabi why awe na jina kubwa ilihali hakupitia ujinga/ukiritimba wa namna hii?

Serikali imedhamini vijana wengi tu kupitia bodi ya mikopo hizo pesa zinarudishwaje kama hizi product walizo zilipia mapesa mengi zimefungwa mikono?

Mbunge Kishimba amewahi toa hoja bungeni kwamba kama Masai anaweza tembeza na kuuza dawa mbalimbali na wala hapati shida toka kwa mamlaka, inakuaje kijana ambae amekaa darasani miaka 5, intern miaka 1, jumla miaka sita ashindwe hata kutoa huduma kwa jamii inayo mzunguka? Wabunge nafikiri hawakumuelewa vizuri!

Waziri wa afya unayo nafasi, Rais unayo nafasi ya kuweka hili jambo sawa, yaani serikali inafanya jitihada kwamba vijana watimize ndoto zao na mwisho wa siku inawanyongelea mbali wale ambao imewahudumia kama sio kutengeneza chuki kwa serikali pitia hivi vyama uchwara nini?

J. Mhagama (MP na waziri) chukua hili na lifanyie kazi sina shaka na wewe.

Thanks, by 4 7mbatizaji
MCT si chama cha madaktari bali ni baraza la Madatari Tanzania, Chama cha Madaktari ni MAT, kuna tofauti kubwa kwa kazi za hivi vyombo viwili
 
Mkuu ndiyo maana nikasema kwamba baraza la madaktari Tangayika (MCT) ni vyema wakafanya tathmini ya hicho wanachofanya kama kweli kinazalisha madaktari mahiri au ipo tu!?

Kwa hayo hayo malengo waliojiwekea kwamba mitihani hiyo itawafanya wao wapate madaktari mahiri basi waangalie kama yamefikiwa.
Huo mtihani unatoa uhakika gani kuwa akifaulu atakuwa mahiri siku zote kwenye performance? Mtihani wa karatasi ni nadharia tu..bora hata ingekuwa practical..mtu amefanya mitihani mingapi huko alikotoka na amefaulu hadi kamaliza internship..unampa mtihani huu wa nini??? Mambo km haya indirectly yanajenga chuki na visasi vinavyolenga wagonjwa..respect these young Doctors waanze kazi chini ya uangalizi..apewe provisional licence akimaliza internship na full licence baada ya let say mwaka mmoja akiwa chini ya uangalizi kwa mfano kwa kuhesabu hata case alizoattend eg minor surgery.. pale anapofanyia kazi..ngp ni nzr na ngp si nzr t s much better kuliko kuwalipisha wafanye mtihani nadharia! Mambo ya kukopi kwa wengine si lazima yote yawe yanafaa kulingana na mzingira yenu..mengine yanatengeneza matatizo tu!
 
Mitihani ni lazima Ili mtu ahakikiwe kweli anaweza kupatia watu matibabu sawa sawa. Afya za watu si kitu Cha mchezo.
Mitihani ya madaktari ni nchi nyingi sana ipo.
Si lazima kinachofanywa nchi H kitafaa pia kikifanywa nchi J.. km shida ni ujuzi bora watafute namna nyingine si hii ya kufanyisha mtihani watu wameshafanya mitihani mingi huko nyuma na wamefaulu..
 
Back
Top Bottom