Wizara ya Afya: Tatizo la Magonjwa yasiyoambukiza linaongezeka

Wizara ya Afya: Tatizo la Magonjwa yasiyoambukiza linaongezeka

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema katika kipindi cha Julai 2021 - Machi 2022, kumekuwa na ongezeko la watu wanaolazwa kutokana na Magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Kisukari, Shinikizo la Damu na Saratani

Akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2022/23 Bungeni, ametoa Wito kwa Wananchi kufanya mazoezi, kuzingatia ulaji wa Vyakula unaofaa na kufanya Vipimo vya Afya mara kwa mara

Aidha, Wizara ya Afya imeomba Bunge kuidhinisha Bajeti ya Trilioni 1.109 kwa Mwaka 2022/23
 
Hatari sana wapige marufuku hivi vinywaji vikali mitaani hasa vileo vya kuanzia 20 alcoholic na energy drinks


USSR
 
Tatizo vipimo ni bei ghali sana,
Halafu naona amesahau malaria na uti au haya yanambukiza?
 
Hatari sana wapige marufuku hivi vinywaji vikali mitaani hasa vileo vya kuanzia 20 alcoholic na energy drinks


USSR
Wakipiga marufuku unadhani hata hiyo bajeti anayoiomba ataipata?..pombe ndio sehemu inayoingiza kodi nyingi kwenye serikali.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom